Loading...

Gamondi: Wachezaji wanatambua tunahitaji nini katika mchezo wa leo


Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi alisema wachezaji wako vizuri na wapo tayari kwa mchezo huo, wanacheza kwa tahadhari kubwa kwa sababu ya ubora wa mpinzani wao.

Alisema hakuna siri yoyote zaidi ya wachezaji kupambana na mashabiki wao kuwaunga mkono katika kila hali na anaimani ya kufanya vizuri katika michezo miwili iliyosalia leo dhidi ya Tanzania Prisons na fainali ya Kombe la Shirikisho la CRBD Bank dhidi ya Azam FC.

“Tumefanya maandalizi mazuri kuelekea mchezo wetu dhidi ya Tanzania Prisons, wachezaji wanatambua tunahitaji nini katika mchezo wetu wa leo, kuna baadhi ya nyota nitawakosa akiwamo Jonas Mkude,” alisema kocha huyo.

Kocha Mkuu wa Tanzania Prisons, Ahmad Ally, alisema wanafahamu wanakutana na timu bora. Wamefanikiwa kuwaona Yanga walipocheza na Tabora United kwa kuona ubora wao.

“Ili uwe bora lazima ukamfunge aliyekuwa bora, ninawaheshimu na kuwapa nafasi wao na kucheza mpira kwa umakini na kuwapa presha, tunajua uhitaji wa hii mechi na sasa ligi imekuwa mgumu hasa nani anayecheza play off.

Ukiangalia msimamo unaona hakuna mwenye uhakika wa kubaki kwenye ligi kulingana na mtu anayeshika nafasi ya tano anaweza kuporomoka hadi chini asipokuwa makini katika mchezo huu wa leo, tunahitaji kupambana kutafuta matokeo mazuri,” alisema Ahmad.
Gamondi: Wachezaji wanatambua tunahitaji nini katika mchezo wa leo Gamondi: Wachezaji wanatambua tunahitaji nini katika mchezo wa leo Reviewed by Zero Degree on 5/28/2024 07:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.