Antonio Conte amemtaja nahodha mpya wa Chelsea rasmi
Conte akiwa na aliyekuwa nahodha wa Chelsea, John Terry |
Antonio Conte amethibittisha kwamba, Gary Cahill atakuwa nahodha mpya wa klabu ya Chelsea.
Beki huyo mwenye mri wa miaka 31, ameiongoza Chelsea kama nahodha kwa sehemu kubwa msimu uliopita wakati John Terry alipokuwa benchi, na sasa amepewa majukumu hayo mojja kwa moja.
Muingereza huyo alijiunga na Chelsea akitokea Bolton Wanderers Januari ya mwaka 2012 na amefanikiwa kushiriki jumla ya mechi 239 kwa klabu hiyo katika mashindano yote ndani ya kipindi cha misimu yake mitano Stamford Bridge.

“Nafikiri kuwa ni jambo sahihi kuendelea na Cahill, kama akicheza, ni vema akiwa kama nahodha,” Conte aliimbia 'The Evening Standard'. “Hiyo ni kwanini? Ni kwa sababu amekaa Chelsea kwa miaka mingi na amecheza michezo mingi na kuonyesha sifa za kupewa nafasi hiyo.”
“Pia, nadhani mbeleni tunaweza kuwa na manahodha wengine ndani ya klabu yetu, anaweza kuwa [Cesar] Azpilicueta, [David] Luiz, na pia, miaka ijayo, inaweza kuwa Thibaut Courtois au Cesc Fabregas,” alisema.
Antonio Conte amemtaja nahodha mpya wa Chelsea rasmi
Reviewed by Zero Degree
on
7/24/2017 09:11:00 AM
Rating: