Loading...

Kambole aiponza Yanga SC


Yanga ilimtambulisha Kambole Juni 16, 2022 akitokea Kaizer Chiefs ambapo Septemba, 2022 iliachana na mchezaji huyo na kumpeleka kwa mkopo kwenye timu ya Wakiso Giant ya Uganda. Kambole Hakucheza mechi yeyote ya kimashindano akiwa ndani ya Yanga kwani alipata majeruhi katika mechi za kirafiki wakati timu hiyo ikijiandaa na msimu mpya wa 2022/2023.

Klabu ya Yanga, imefungiwa kusajili mpaka itakapomlipa aliyekuwa mchezaji wake Lazarus Kambole. Uamuzi huo umefanywa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) baada ya mchezaji huyo kushinda kesi ya madai dhidi ya klabu hiyo.


Mchezaji huyo raia wa Zambia alifungua kesi FIFA akidai malipo ya malimbikizo ya mishahara na fidia ya kuvunjiwa mkataba. Yanga ilitakiwa iwe imemlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa, lakini haikutekeleza hukumu hiyo.


Wakati FIFA imeifungia klabu hiyo kufanya uhamisho wa wachezaji kimataifa, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) nalo limeifungia kufanya uhamisho wa ndani.
Kambole aiponza Yanga SC Kambole aiponza Yanga SC Reviewed by Zero Degree on 5/01/2024 11:00:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.