Loading...

Marufuku kuvuta sigara hadharani - Dk. Mollel



Serikali kupitia Wizara ya Afya imesema tayari bunge limepitisha Sheria ya Udhibiti wa Tumbaku ijulikanayo kama “The Tobacco Products (Regulation) Act, 2003” ambayo imetoa katazo la uvutaji wa Sigara hadharani.

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel alibainisha hayo jana Aprili 30,2024 Jijini Dodoma wakati akijibu swali Namba 215 kutoka kwa Mbunge wa Tumbe, Mhe. Amour Khamis Mbarouk aliyeuliza Je, ni lini Serikali italeta Sheria ya Kuzuia uvutaji wa sigara na mazao mengine hadharani.

Aidha amesema sheria hiyo imezuia matangazo ya tumbaku na bidhaa zitokanazo na tumbaku kwenye maeneo ya umma ikiwemo vyombo vya habari, billboards na kwenye matamasha mbalimbali.
Marufuku kuvuta sigara hadharani - Dk. Mollel Marufuku kuvuta sigara hadharani - Dk. Mollel Reviewed by Zero Degree on 5/01/2024 10:32:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.