Loading...

Lissu amjibu Fatma Karume


Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Bara, Tundu Lissu, amesema hajafanya makosa kumuita Mzanzibar Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwa ndiyo asili yake.

Lissu ametoa kauli hiyo jana tarehe 29 Aprili 2024, jijini Dodoma, akizungumza katika mkutano wa hadhara, akimjibu mwanaharakati Fatma Karume, aliyemuita mbaguzi kufuatia hatua yake ya kumtambulisha Rais Samia Mzanzibar wakati anamkosoa.

“Nataka niseme ubaguzi wangu na katiba ya Zanzibar inavyosema, kwenye katiba ya Zanzibar inasema kutakuwa na Mzanzibar haisemi tutakuwa na Mtanzania wa Tanganyika, inasema kutakuwa na Mzanzibar na inasema kila Mzanzibar atafaidi haki na fursa anazostahili Mzanzibar,” amesema Lissu.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X, jana Jumapili, Fatma alihoji iwapo sera ya Chadema ni kutokuwa na Rais wa Tanzania kutoka Zanzibar, baada ya Lissu kusema kuna Rais Samia ni Mzanzibar na sio Mtanganyika.

“Kuna tofauti kubwa baina ya siasa za hoja na siasa za ubaguzi. Tundu, hizi ni siasa za ubaguzi. Ni opportunism na siasa hizi zinaleta manufaa ya mpito tu. Swali, kwani sera ya Chadema ni kutokuwa na Rais wa Tanzania kutoka Zanzibar milele?” alihoji Fatma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Lissu amjibu Fatma Karume Lissu amjibu Fatma Karume Reviewed by Zero Degree on 5/01/2024 10:30:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.