Loading...

Mkataba wa TANESCO na SONGAS kumalizika Julai 2023

Naibu Waziri Wizara ya Nishati, Judith Kapinga

Serikali imesema kuwa mkataba wa ununuzi wa umeme kati ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na SONGAS utafikia ukomo Julai 31 mwaka huu, na kwamba wameunda timu ya wataalam (Government Negociation Team - GNT) iliyoanza majadiliano mwezi Aprili, 2023 na inatarajia kukamilisha majadiliano hayo kabla ya mkataba kuisha.

Hayo yamesemwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga wakati akijibu swali la Mbunge Jesca Kishoa aliyetaka kujua makubaliano ya mkataba ujao kati ya SONGAS na Serikali yamefikia hatua gani ikiwa mkataba wa awali upo katika mwaka wa mwisho.

Naibu Waziri Kapinga amesema kuwa Serikali itahakikisha maslahi ya Taifa yanazingatiwa kabla ya makubaliano yatakayofuata.
Mkataba wa TANESCO na SONGAS kumalizika Julai 2023 Mkataba wa TANESCO na SONGAS kumalizika Julai 2023 Reviewed by Zero Degree on 5/27/2024 11:37:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.