Loading...

Rufaa ya Ole Sabaya, wenzake yaondolewa

Lengai Ole Sabaya

Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) amewasilisha Mahakama Kuu ya Tanzania masijala ndogo ya Arusha, nia ya kutoendelea na rufaa dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake watano.

Kufuatia nia hiyo, Mahakama imeridhia na kuondoa rufaa hiyo ya jinai namba 155/2022 na kufuatia uamuzi huo, Sabaya anakuwa hana shauri lolote linalomkabili mahakamani na anahitimisha rasmi safari ya kesi alizokuwa anakabiliana nazo kuanzia Juni 4,2021 alipopandishwa kizimbani mara ya kwanza.

Rufaa hiyo iliyokuwa imepangwa kusikilizwa leo Mei 3, 2024, ikipinga hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha katika kesi ya uhujumu uchumi namba 27/ 2021, iliyowaachia huru Sabaya na wenzake.

Notisi hiyo imewasilishwa leo na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Akisa Mhando, mbele ya Jaji Salma Maghimbi.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya uamuzi huo, Wakili Mosses Mahuna aliyekuwa akiwawakilisha Sabaya na wenzale, amesema kwa sasa Sabaya na wenzake wako huru na hawakabiliwi na shauri lolote mahakamani.
Rufaa ya Ole Sabaya, wenzake yaondolewa Rufaa ya Ole Sabaya, wenzake yaondolewa Reviewed by Zero Degree on 5/03/2024 09:53:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.