Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 2 Mei, 2024

Gabriel Jesus, 27

Klabu ya Arsenal wako tayari kupokea ofa ya kumuuza mshambuliaji wao wa Brazil Gabriel Jesus, 27, wakati wa majira ya joto ya msimu huu.

Klabu ya Manchester United wanapanga kubaki na kocha wao Erik ten Hag msimu ujao kwa sababu ya kukosekana kwa mbadala wake, pamoja na gharama ya kumuondoaMholanzi huyo. (Athletic)

Washika bunduki wana matumaini kuwa kiungo wa kati wa Italia Jorginho, 32, atapuuza nia ya Juventus, Lazio na Napoli kutaka kumsajili na kusaini mkataba wa nyongeza. (Standard)

Brighton watajaribu kumnunua Kieran McKenna kutoka Ipswich Town ikiwa meneja Roberto de Zerbi ataondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu. (Guardian)

Bruno Fernandes, 29

Kiungo wa kati wa Manchester United na Ureno Bruno Fernandes, 29, anasema mustakabali wake Old Trafford utategemea ikiwa klabu hiyo itamtaka abaki.

Klabu ya Tottenham wanawasaka kiungo wa kati wa Chelsea na England Conor Gallagher, 24, pamoja na mshambuliaji wa Feyenoord mwenye umri wa miaka 23 na Mexico Santiago Gimenez msimu huu wa joto, huku pia wakimfuatilia mlinzi wa Bournemouth raia wa Uingereza Lloyd Kelly, 25. (Telegraph).

Everton huenda wakalazimika kumuuza mlinda lango wa England Jordan Pickford, 30, iwapo pendekezo lao kununuliwa na wamiliki wapya 777 Partners litaporomoka. (Talksport)

Everton inawafuatilia beki wa Hull City Muingereza Jacob Greaves, 23, na mshambuliaji wa Blackburn Rovers' Jamhuri ya Ireland Sammie Szmodics, 28.

Amadou Onana, 22

Arsenal, Bayern Munich na Newcastle ni miongoni mwa klabu zilizopewa nafasi kubwa ya kumsajili kiungo wa kati wa Everton na Ubelgiji Amadou Onana, 22. (Football Transfers)

Newcastle United haitashinikizwa kumuuza kiungo wa kati wa Brazil Bruno Guimaraes, 26, chini ya kifungu chake cha pauni milioni 100 au kuachana na mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak, 24. (i Sport)

Newcastle wanakaribia kumsajili beki wa Fulham mwenye umri wa miaka 26 Tosin Adarabioyo kwa uhamisho wa bure. (Sun)

Adarabioyo, ambaye pia anawaniwa na AC Milan, Manchester United na Liverpool, ameifahamisha Fulham kwamba hatasaini mkataba mpya wakati mkataba wake wa sasa utakapokamilika msimu huu wa joto. (Mail)

Jurgen Klopp

Borussia Dortmund wanafikiria kumrejesha kocha wa zamani Jurgen Klopp kama mkuu wa soka mwaka 2025 baada ya meneja huyo wa Liverpool kuondoka Anfield mwishoni mwa msimu huu. (Independent)

Klabu ya West Ham wanamtarajia kiungo wa kati wa Ghana Mohammed Kudus, 23, kiungo wa kati wa Brazil Lucas Paqueta, 26, na kiungo wa kati wa Mexico Edson Alvarez, 26, kushinikiza kuondoka katika klabu hiyo msimu huu. 

Meneja msaidizi wa Feyenoord Sipke Hulshoff, mkuu wa utendaji Ruben Peeters na mchambuzi Etienne Reijnen wamekubali kumfuata kocha Arne Slot kwenda Liverpool. (Football Insider)

Fluminense wamewasilisha pendekezo rasmi la kutaka kumsajili beki wa Brazil Thiago Silva baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 39 kutangaza kuwa ataondoka Chelsea mwishoni mwa msimu huu. (Fabrizio Romano)

Beki wa Barcelona na Uruguay Ronald Araujo, 25, anatathmini iwapo atasaini mkataba mpya na klabu hiyo ya Uhispania huku Manchester United na Bayern Munich zikiwa na nia ya kumsajili. (Sport)
Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 2 Mei, 2024 Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 2 Mei, 2024 Reviewed by Zero Degree on 5/02/2024 09:23:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.