Loading...

Walter: Utendaji bora ulinileta Yanga


MENEJA wa Yanga, Walter Harson amesema utendaji wake bora kwenye tasnia ya habari ni sababu ya Rais wa Yanga, Hersi Said kumpa ulaji klabuni hapo.

Julai 31, 2022 Yanga ilitangaza kumuajiri Walter Harson kuwa meneja wa klabu hiyo.

Akizungumza na mtandao huu, Walter Harson amesema utendaji wake ulianza kuonekana akiwa Azam TV ambako alikuwa mchambuzi wa michezo na baadaye klabu ya KMC kama Mkurugenzi Mtendaji kisha kuajiriwa Yanga.

“Hakuna njia rahisi yoyote zaidi ya juhudi ambazo nimezifanya za utendaji,” amesema Walter.

Pia meneja huyo amesifu idara zingine ndani ya klabu hiyo kwa namna zinavyoendelea kupiga hatua nzuri kila kukicha, ikiwemo idara ya fedha, habari, sheria na zingine.

Cc: Habari leo
Walter: Utendaji bora ulinileta Yanga Walter: Utendaji bora ulinileta Yanga Reviewed by Zero Degree on 5/02/2024 10:52:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.