Loading...

Lusajo awapiku Azizi Ki, Feitoto


Wakati Kaimu Mkuu wa Simba, Juma Mgunda, akiteuliwa kuwa Kocha Bora wa Mei, straika wa Mashujaa FC ya Kigoma, Reliants Lusajo, ametwaa tuzo ya Mchezaji Bora akiwabwaga, Stephanie Aziz Ki wa Yanga na Feisal Salum 'Fei Toto' kutoka Azam FC.

Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi jana imesema, Mgunda aliwashinda Miguel Gamondi wa Yanga na Bruno Ferry wa Azam FC.

Mgunda aliiongoza Simba kukusanya pointi 19 katika michezo saba iliyocheza, ikishinda sita na kutoa sare moja.

Iliifunga Tabora United na JKT Tanzania mabao 2-0, mabao 3-0 dhidi ya Azam FC, KMC na Dodoma Jiji bao 1-0, Geita Gold mabao 4-1, na sare ya bao 1-1 dhidi ya Kagera Sugar.

Lusajo, aliyesajiliwa na Mashujaa akitokea Namungo, aliwazidi Aziz Ki na Fei Toto, ambao waliingia katika hatua ya fainali ya kuwania tuzo ya mwezi huo huku akiifungia timu yake mabao matano na kuhusika kwenye 'asisti' mbili kwenye mechi za hatua ya lala salama.

Tuzo za jumla zinazotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), zitafanyika mapema kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa mashindano.
Lusajo awapiku Azizi Ki, Feitoto Lusajo awapiku Azizi Ki, Feitoto Reviewed by Zero Degree on 6/05/2024 07:32:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.