Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 14 Juni, 2024

Virgil van Dijk kuwa beki anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani

Klabu ya Al Nassr inayoshiriki ligi ya Saudi Pro, inataka kumfanya beki wa Liverpool na timu ya taifa ya Uholanzi Virgil van Dijk kuwa beki anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani. (Marca)

Klabu ya Newcastle na Bayern Munich zilikuwa klabu za kwanza kuwasiliana na Crystal Palace zikitaka kumsajili winga Mfaransa Michael Olise, mwenye umri wa miaka 22.

Liverpool na Manchester United zote zinamsaka beki wa kati wa Lille Mfaransa Leny Yoro, 18, lakini Real Madrid pia wanamtaka. (Athletic)

Chelsea nao walifuata mkondo kuwasiliana na Palace kuhusu Olise, na kuwafikia siku ya Alhamisi. (Mirror)

Klabu ya Manchester United inamfuatilia kwa karibu beki wa Bayern Munich na Uholanzi Matthijs de Ligt, 24. (Sky Sports Germany)

Manchester United pia ina Mfaransa Jean-Clair Todibo mwenye umri wa miaka 24 wa Nice, klabu nyingine inayomiliki Ineos, kama chaguo wanapotaka kuajiri beki. (Mail)

Mshambuliaji wa Bologna Mholanzi Joshua Zirkzee, 23, pia yuko kwenye rada za Manchester United msimu huu wa joto, lakini wanaweza kukabiliwa na ushindani kutoka kwa AC Milan na Juventus.

Mshambuliaji wa Roma na timu ya taifa ya Uingereza, Tammy Abraham

Klabu za Tottenham, Aston Villa na West Ham zinavutiwa na mshambuliaji wa Roma na England Tammy Abraham, 26. (Telegraph)

Aston Villa wanahitaji pauni milioni 40 kumnunua mshambuliaji Jhon Duran, huku Chelsea wakiwa kwenye mazungumzo ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20. Raia huyo wa Colombia amecheza mechi tatu pekee za Ligi ya Primea tangu ajiunge nao Januari 2023. (Times)

Mkufunzi mpya wa klabu ya Fenerbahce Jose Mourinho anataka kumsajili kiungo wa kati wa Denmark Pierre-Emile Hojbjerg, 28, kutoka Tottenham. (Takvim)

Klabu ya West Ham na Leicester City wamekutana na wawakilishi wa mshambuliaji wa Juventus Muargentina Matias Soule, 21, mjini London. (Tuttosport)

Arsenal wanakabiliwa na kipingamizi katika harakati zao za kumnunua mshambuliaji wa Sporting Lisbon na Uswidi Viktor Gyokeres, 26, huku hesabu ya timu hiyo ya Ureno ikiwa juu kuliko ile ambayo The Gunners wako tayari kulipa. (Sun)

Klabu ya Brentford haitamuuza mshambuliaji wa Uingereza Ivan Toney, mwenye umri wa miaka 28, kwa chini ya pauni milioni 60, ingawa hapo awali walikadiria thamani yake kuwa pauni milioni 80. (Sportsport)

Mkufunzi wa zamani wa Brighton Roberto de Zerbi anatazamiwa kukubali kandarasi ya miaka mitatu kuwa kocha wa Marseille. Brighton angepokea ada ya euro milioni sita.

Kevin Danso, 25

Klabu za Ligi Kuu ya England zinamtaka beki wa Lens na Austria Kevin Danso, 25, ambaye ameungwa mkono na mchezaji wa zamani Rio Ferdinand kuhamia Manchester United.

Mchezaji wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri chini ya miaka 21 anayeichezea Chelsea Noni Madueke, yuko kwenye orodha ya walioteuliwa kusajiliwa na Newcastle huku klabu hiyo ikiwa na mpango wa kumnunua winga mpya wakati dirisha la uhamisho wa wachezaji litakapofunguliwa. (i Sport))
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 14 Juni, 2024 Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 14 Juni, 2024 Reviewed by Zero Degree on 6/14/2024 07:47:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.