Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 1 Juni, 2024


Borussia Dortmund haiwezi kumudu kumnunua tena winga wa Uingereza Jadon Sancho, 24, kutoka Manchester United kwa mkataba wa kudumu.

Mazungumzo ya Sunderland na bosi wa zamani wa Reims Will Still kuhusu nafasi ya umeneja iliyoachwa wazi yamevunjika. (Sky Sports)

Kiungo wa kati wa Uingereza Kobbie Mainoo, 19, atatia saini mkataba mpya na Manchester United wenye thamani mara nne ya mshahara wake wa sasa baada ya michuano ya Ulaya msimu huu. (Star)

Mshambulizi wa Uingereza Mason Greenwood, 22, anakaribia kujiunga na Juventus kutoka Manchester United.

Klabu ya Everton wako tayari kumuuza mchezaji wao yeyote nyota msimu huu wa majira ya joto, akiwemo mlinda lango wa Uingereza Jordan Pickford, 30, na mlinzi wa Uingereza Jarrad Branthwaite, 21, ambaye analengwa na Manchester United. (Sun)

Nottingham Forest itaweka bei ya £40m kwa kiungo Mwingereza Morgan Gibbs-White, 24, ambaye anafuatiliwa kwa karibu na Tottenham.

Tottenham Hotspur wanaweza kumsajili mshambuliaji wa Uingereza Ivan Toney, 28, kwa mkataba wa thamani ya £40m kutoka Brentford msimu huu. (Football Insider)

Kiungo wa kati wa Real Sociedad na Uhispania Martin Zubimendi, 25, hana nia ya kujiunga na Arsenal licha ya The Gunners kuonyesha nia ya kumtaka. (Sport)

Klabu ya Napoli wamefikia makubaliano na Antonio Conte kwa kocha huyo wa zamani wa klabu ya Chelsea na Tottenham kuwa meneja wao mpya. (Fabrizio Romano)

Galatasaray wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Ujerumani na Barcelona Ilkay Gundogan, 33, ili kuimarisha kikosi chao kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. (90min)

Ousmane Diomande, 20

Manchester United wanaweza kutaka kumnunua mlinzi wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 20 Ousmane Diomande kutoka Sporting Lisbon. (Express)

Kipa wa Brazil Ederson, 30, anaendelea kuhusishwa na kuhamia Saudi Arabia lakini atalazimika kuomba uhamisho ikiwa anataka kuondoka Manchester City. (ESPN)

Ni Paris St-Germain pekee inayoweza kumudu mshahara wa Anthony Martial mwenye umri wa miaka 28 ikiwa fowadi huyo ataamua kurejea kwao Ufaransa baada ya kuondoka Manchester United. (Foot Mercato)

Vilabu vya Saudi Pro League vinaweza kuwa tayari kulipa euro 100m (sawa na pauni 85m) kumsajili winga wa Brazil Raphinha, 27, kutoka Barcelona. (Mundo Deportivo)

Eintracht Frankfurt wanataka kumsajili kiungo wa kati wa klabu ya Brighton wa Ujerumani Pascal Gross, 32, lakini hawajaondoa uwezekano wa uhamisho wa kiungo wa kati wa Uingereza Kalvin Phillips, 28, kutoka Manchester City. (Sky Sports Germany)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 1 Juni, 2024 Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 1 Juni, 2024 Reviewed by Zero Degree on 6/01/2024 09:16:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.