Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 3 Juni, 2024
Mshambulizi wa klabu ya Napoli na Nigeria Victor Osimhen, mwenye umri wa miaka 25, anasubiri ofa kutoka kwa Arsenal au Saudi Arabia. (Gazzetta dello Sport)
Bayern Munich wanataka kumsajili Bruno Fernandes, Jadon Sancho anaweza kuichezea tena Manchester United na Victor Osimhen anasubiri ofa kutoka kwa Arsenal.
Bayern Munich wanatafuta saini ya kiungo wa kati wa Ureno Bruno Fernandes, 29, kutoka Manchester United. (O Jogo)
Palace italenga kumsajili winga wa Leeds Mholanzi Crysencio Summerville mwenye umri wa miaka 22, ikiwa itabidi kumuuza Olise au Eze msimu huu wa joto.
Jadon Sancho, mwenye umri wa miaka 24, yuko tayari kurejea United kufuatia kipindi cha mkopo cha winga huyo wa Uingereza katika klabu ya Borussia Dortmund - lakini tu ikiwa Erik ten Hag ataondoka msimu huu wa joto. (Mirror)
Kiungo wa kati wa Ubelgiji Kevin de Bruyne, ambaye atafikisha miaka 33 baadaye mwezi huu, anatarajiwa kupokea ofa za kuondoka Manchester City msimu huu wa joto.
Mkufunzi wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson amekutana na mkurugenzi wa michezo wa Crystal Palace Dougie Freedman mjini London kuchunguza msimamo wao kuhusu uwezekano wa kuwauza beki wa Uingereza Marc Guehi, 23, kiungo wa kati wa Uingereza Eberechi Eze, 25, na winga wa Ufaransa aliye Michael Olise 22, msimu huu wa joto.
Klabu ya Tottenham wanaweza kuwasilisha ofa kwa winga wa Nottingham Forest na timu ya taifa ya Uingereza Callum Hudson-Odoi, 23, kabla ya mwisho wa mwezi. (Football Insider)
Cristiano Ronaldo amezungumza na wachezaji wenzake wawili wa zamani kwa lengo la kuwashawishi wajiunge naye katika klabu ya Al Nassr - beki wa Real Madrid na Uhispania Nacho Fernandez, 34, na kiungo wa kati wa Manchester United na Brazil Casemiro, 32. (Marca)
Fulham wamemweka Emile Smith Rowe wa Arsenal kuwa mojawapo ya vipaumbele vyao vya uhamisho wa majira ya joto na wako tayari kuwasilisha ofa kwa kiungo huyo wa kati wa Uingereza, mwenye umri wa miaka 23, mapema katika kipindi cha uhamisho.
Newcastle United itajaribu kukamilisha mpango wa kumnunua beki wa kati wa Bournemouth Lloyd Kelly, 25, wiki hii. (Telegraph)
Klabu ya West Ham wamekaribia kuafikia mkataba wa pauni milioni 25.5 kumsaini mshambuliaji wa Brazil Luis Guilherme kutoka Palmeiras , 18. (Times)
Los Angeles Galaxy wametuma ofa ya mkataba kwa kiungo wa zamani wa Ujerumani Marco Reus, 35, ambaye anatazamiwa kuwa mchezaji huru baada ya kucheza mechi yake ya mwisho Borussia Dortmund.
Kocha wa Leicester City Enzo Maresca atatangazwa kuwa kocha mpya wa Chelsea siku ya Jumatatu, baada ya kusaini mkataba wa miaka mitano. (Fabrizio Romano)
Kocha wa zamani wa Chelsea na Tottenham Antonio Conte anatarajiwa kuteuliwa kuwa kocha mpya wa Napoli wiki hii. (Nicolo Schira)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 3 Juni, 2024
Reviewed by Zero Degree
on
6/03/2024 08:09:00 AM
Rating: