Loading...

Kinana ajiuzulu CCM, Rais Samia aridhia


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi la kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM, Abdulrahman Kinana ambaye amemwandikia barua ya kuomba kupumzika.

Katika majibu yake Mwenyekiti wa CCM amesema “Ni kweli nilipokuomba utusaidie kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti nilikuahidi utakaa muda mfupi kama ulivyoomba, na kwa kweli nilipenda uendelee kutusaidia lakini kwa kuwa umeomba sana na ahadi ni deni
nalazimika kwa moyo mito kuridhia kujiuzulu kwako”.

Pia Mwenyekiti wa CCM amesisitiza kuwa Chama kitaendelea kutumia uzoefu na maarifa ya Kinana kila vitakapohitajika na kwamba chama cha Mapinduzi kinamshukuru Kinana kwa mchango wake mkubwa kwa Chama chao.
Kinana ajiuzulu CCM, Rais Samia aridhia Kinana ajiuzulu CCM, Rais Samia aridhia Reviewed by Zero Degree on 7/30/2024 07:09:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.