Korea Kaskazini yakumbwa na mafuriko
![]() |
Picha na vyombo vya habari vilionyesha Kim akisafiri ndani ya gari jeusi aina ya Lexus katika eneo lenye maji ya mafuriko |
Mvua iliyovunja rekodi imesababisha maelfu ya watu kukwama kutokana na mafuriko nchini Korea Kaskazini mwishoni mwa juma, na kumfanya Kim Jong Un kutangaza "dharura", vyombo vya habari vya serikali vinaripoti.
Picha zinaonyesha mashamba na nyumba zilizozama baada ya mvua kubwa kuathiri jiji la Sinuiju na kaunti ya Uiju, ambayo inapakana na China, kulingana na Rodong Sinmun.
Vyombo vya habari vya serikali vimesema kuwa wengi waliokolewa baadaye kwa ndege, ingawa BBC haikuweza kuthibitisha kwa uhuru maelezo ya ripoti hiyo.
Korea Kaskazini yakumbwa na mafuriko
Reviewed by Zero Degree
on
7/29/2024 06:21:00 PM
Rating:
