Loading...

Uganda imethibitisha kugunduliwa kwa wagonjwa Homa ya Nyani nchini humo


Wizara ya afya nchini Uganda imethibitisha kugunduliwa kwa kesi mbili za maradhi ya Homa ya Nyani {Mpox} nchini humo.

Kulingana na taarifa iliotumwa kwa vyombo vya habari na mkurugenzi wa habari katika wizara ya afya nchini humo, maradhi hayo yalibainika baada ya kuchukuliwa sampuli kutoka kwa wagonjwa wawili.

Taarifa hiyo inasema wawili hao ni mwanamke mmoja wa miaka 37 kutoka baraza la manispaa ya mpondwe ambaye ameolewa na mwanamume raia wa DR Congo na mwanamke mwengine mwenye umri wa miaka 22 raia wa DR Congo kutoka kijiji cha Bunywisa II katika wilaya ya Kasese.Wote wawili walikuwa na upele katika ngozi zaona dalili zinazohusishwa na homa ya nyani.

Taarifa hiyo inaongezea kwamba sampuli za wawili hao zilifanyiwa ukaguzi na Taasisi ya kupima virusi nchini Uganda UVRI tarehe 24 mwezi Julai 2024.Kesi za maradhi hayo ni miongoni mwa sita zilizogunduliwa katika mpaka wa Bwera wilayani Kasese.

Matokeo ya ukaguzi huo yamebaini kwamba maambukizi hayo hayakufanyika nchini Uganda na kufikia sasa hakuna maambukizi yaliotokana na visa hivyo viwili.

Tayari wizara ya Afya nchini Uganda imepeleka timu ya maafisa wa kukabiliana na dharura katika Wilaya ya Kasese ili kushirikiana na maafisa wa afya katika eneo hilo ili kudhibiti visa hivyo viwili.

Kufikia sasa watu tisa wanaodaiwa kushikana kimwili na waathiriwa wanafuatiliwa kwa karibu.

Uganda inaendelea kufuatialia kwa karibu mambukizi ya maradhi hayo nchini DR Congo ambapo imatengazwa kwamba karibu mikoa yote imeripoti visa vya maambukizi , huku mkoa wa hivi karibuni ukiwa ule wa Kivu Kaskazini hususan mjini Goma.
Uganda imethibitisha kugunduliwa kwa wagonjwa Homa ya Nyani nchini humo Uganda imethibitisha kugunduliwa kwa wagonjwa Homa ya Nyani nchini humo Reviewed by Zero Degree on 8/02/2024 04:14:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.