Florent Ibenge ndiye kocha mkuu mpya wa Azam FC
Azam FC imemtambulisha Florent Ibenge, raia kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili.
Kabla ya kusaini mkataba na klabu ya Azam FC, Florent Ibenge amewahi kuvinoa vilabu mbalimbali vya Afrika ikiwemo RS Berkane, Al-Hilal Club, AS Vita na Timu ya Taifa ya DRC.
Zoezi la utiaji saini mkataba kati ya Ibenge na Azam FC lilishuhudiwa na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Azam, Abdulkarim Shermohamed.
Florent Ibenge ndiye kocha mkuu mpya wa Azam FC
Reviewed by Zero Degree
on
7/05/2025 10:20:00 PM
Rating:
