Serikali ya Tanzania imeanzisha Bima ya safari kwa raia wa kigeni
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Sheria ya Bima, Sura ya 394 imeanzisha bima ya safari kwa raia wa kigeni wanaoingia Tanzania Bara kwa kulipa ada ya bima kwa shilingi ya Tanzania yenye thamani sawa na dola za Marekani 44.
Lengo la Bima hii ni kwa ajili ya matibabu ya dharura kwa wageni wanapokuwa hapa nchini, kupotea kwa mizigo ya wageni, huduma za uokoaji na kurudishwa kwa mgeni nchini kwake iwapo hali ya dharura itatokea.
Ukataji wa Bima kwa raia wa kigeni wataoingia nchini utaanza rasmi baada ya kanuni za usimamizi wa bima ya safari kuchapishwa kwenye Gazeti la Serikali. Umma utajulishwa hatua hiyo itakapokamilika.
Taarifa kamili hiyo hapo chini:
Serikali ya Tanzania imeanzisha Bima ya safari kwa raia wa kigeni
Reviewed by Zero Degree
on
7/04/2025 07:42:00 PM
Rating:
