Vitu viwili vya kupunguza kasi ya mafuta ghafi EACOP kujengwa nchini
*📌Vinalenga kupunguza kasi ya Mafuta kutoka Hoima Uganda hadi Chongoleani Tanzania*
*📌Ujenzi wafikia asilimia 50*
*📌 Mabomba ya kipenyo cha inchi 24 kutumika kusafirsha mafuta ghafi*
📌 *Wataalam wazawa waomba Serikali kuwa na data za kuwatambua pindi miradi inapotokea*
Jumla ya vituo viwili vya kupunguza kasi ya mafuta ghafi yanayotoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani - Tanga vinatarajia kujengwa ili kusaidia upunguzaji wa kasi ya mafuta ghafi yanayosafirishwa sambamba na kulinda miundombinu ya bomba hilo la mafuta.
Hayo yamesemwa na Mtaalamu wa Ujenzi wa Miundombinu hiyo kutoka kituo namba moja (PRS-1) inayojengwa Kata ya Kibaya, Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara. Mhandisi Damian Lasway, wakati alipokuwa akizungumzia maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya kituo hicho ambapo amesema ujenzi wa kituo umefikia asilimia 50.
Amesema ujenzi wa vituo hivyo utaenda sambamba na wa nchini Uganda, ambapo kwa hapa nchini vituo hivyo viwili vitajengwa sambamba na vile vya kusukuma mafuta vitakavyojengwa Muleba, Mbogwe, Igunga na Singida na vingine viwili vitakuwa nchini Uganda.
‘’kazi hii ya ujenzi wa vituo hivi ni muhimu sana kwani mafuta yakiwa yanasafiri kutoka Uganda yanakuwa na kasi kubwa hivyo ni lazima kuwe na kituo cha kupunguza presha hiyo ya mafuta na baadae yaendelee kusafiri ‘’ ameisema Mha. Lasway.
Amesema kituo cha kwanza kitajengwa mkoani Manyara, Kata ya Kibaya, Wilaya ya Kiteto na cha pili kitajengwa Kata ya Sindeni , Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga.
Ameongeza kuwa, Tanzania na Uganda zimefanya kazi kubwa kwenye utekelezaji wa mradi huo wa bomba la mafuta ghafi kwa kuhakikisha wazawa wananufaika na ujuzi kutoka kwa wataalamu mbalimbali wa kimataifa kutoka nchi tofauti.
Akizungmzia namna wanavyonufaika na ujuzi huo, baadhi ya wazawa wanaofanyakazi kwenye eneo hilo akiwemo Rajab Rajab ambaye ni mhakiki ubora PRS-1 amesema kwa sasa uwezo wao umekua kwa kiasi kikubwa tofauti na ilivyokuwa awali wakati wanaingia kwenye mradi.
‘’Nina uhakika ukitokea mradi kama huu tena tutakuwa na uwezo mkubwa wa kutekeleza miradi jambo kubwa ni kwa Serikali kututambua na kuweka data za wataalamu ili zinapohitajika zipatikane kwa urahisi’’ Amesema Rajab.
Naye Afisa Rasilimali Watu bi. Priscilla Baregu amesema licha ya wazawa kupewa kiqumbele kwenye utekelezaji wa mradi huu, tayari wameanza kuwatambua wafanyakazi wasio na ujuzi kwa kuwapeleka kwenye vyuo vinavyotambulika na kupatiwa mafunzo rasmi.
‘’Mpaka sasa tumeshawapeleka wafanyakazi takribani 4 kwenye mafunzo rasmi na tunawagharamia kila kitu ili kutoa motisha na kuwa na weledi mpindi mradi utakapomalizika’’ Amesema Bi. Priscilla.
Mradi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki utatekelezwa kwa vipande 16 ambapo cha kwanza kinaanzia nchini Uganda kuelekea Chongoleani Tanga.
Vitu viwili vya kupunguza kasi ya mafuta ghafi EACOP kujengwa nchini
Reviewed by Zero Degree
on
7/24/2025 09:27:00 AM
Rating:
