Loading...

Waziri Mkuu Majaliwa kufungua CHAN2024 kwa Mkapa


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mashindano ya CHAN 2024, yanayotarajiwa kuanza rasmi Agosti 02, 2025 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Amebainisha hayo Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msingwa Julai 28, 2025 jijini Dar es Salaam wakati akikagua maandalizi ya Ufunguzi huo.

Amesema kuwa, nchi 5 za Afrika ambazo ni Burkinafaso, Algeria, Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Maurtania, Madagascar tayari zimeanza kuwasili kuanzia Julai 28,2025.

"Kabla ya uzinduzi huo, uwanja utapambwa na burudani za Mziki ambazo zitahusisha wasanii wa Singeli (CHAN SINGELI FEST) ambalo litafanyika nje ya Uwanja wa Benjamin Mkapa, bila kiingilio, kuanzia Julai 30 hadi 31, 2025" alisema Msigwa.

Ameongeza kuwa, mashindano hayo ni moja ya maandalizi ya kuelekea kuwa wenyeji wa AFCON 2027, hivyo ni nafasi nzuri ya kufanya maandalizi ikiwemo kuwakaribisha wageni kwani njia za kuingia nchini zimerahisishwa.







Waziri Mkuu Majaliwa kufungua CHAN2024 kwa Mkapa Waziri Mkuu Majaliwa kufungua CHAN2024 kwa Mkapa Reviewed by Zero Degree on 7/28/2025 01:31:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.