Loading...

UEFA yaiadhibu Manchester City


SHIRIKISHO la Soka la Ulaya (Uefa) limeipiga faini klabu ya Manchester City baada ya mashabiki wake “kutupa vitu “ wakati wakishinda 2-0 mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya dhidi ya Dinamo Zagreb Jumanne.

Zagreb pia nao wameshitakiwa kwa kosa kama hilo pamoja na kutakiwa kulipa gharama ya uharibifu kwenye Uwanja wa Etihad Stadium. Kesi hiyo itasikilizwa na Uefa Oktoba 17 mwaka huu.

Timu ya Ugiriki ya Olympiakos yenyewe imeshtakiwa kwa kosa la kufanya vitendo vya kiubaguzi kupitia mabango wakati timu yao ilipofungwa 3-1 na Red Star Belgrade. Kesi hiyo ilitarajia kusikilizwa jana, Oktoba 4.
UEFA yaiadhibu Manchester City UEFA yaiadhibu Manchester City Reviewed by Zero Degree on 10/06/2019 02:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.