Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 14 Julai, 2024


Manchester City wamepokea dau la pauni milioni 25 kutoka kwa Saudi Pro League kwa ajili ya mlinda mlango wa Brazil Ederson mwenye umri wa miaka 30. (HITC)

Klabu ya Manchester United wanataka kumuuza mlinzi wa Uswidi Victor Lindelof, mwenye umri wa miaka 29, msimu huu wa majira ya joto na pia watasikiliza ofa kwa ajili ya kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, mwenye umri wa maiaka 32. (Manchester Evening News)

Chelsea wako tayari kumenyana na Tottenham, Bayern Munich na Paris St-Germain kumnunua kiungo wa kati wa Rennes Mfaransa Desire Doue, 19. (L'Equipe)

Manchester United wanavutiwa na mshambuliaji wa Brentford na England Ivan Toney, 28, ambaye yuko tayari kuhamia Old Trafford. (Christian Falk)

Mlinzi wa Ureno Nuno Tavares, 24, yuko mbioni kujiunga na Lazio kwa mkopo kutoka Arsenal.

Klabu ya Serie A ya Como iko tayari kumsajili mlinzi wa Ufaransa Raphael Varane, mwenye umri wa miama 31, kama mchezaji huru baada ya kuondoka kwake katika klabu ya Manchester United msimu huu. (Fabrizio Romano)

West Ham wameonesha nia ya kutaka kumnunua winga wa Uholanzi Steven Bergwijn, mwenye umri wa miaka 26, lakini Marseille na vilabu viwili vya Saudi Arabia pia vinatumai kumnasa kutoka Ajax. (De Telegraaf)


Klabu ya Atletico Madrid wanatarajiwa kuipa AC Milan idhini ya kumsajili Alvaro Morata, mwenye umri wa miaka 31, wiki ijayo baada ya kukamilisha majukumu yake ya kimataifa na Uhispania kwenye Euro 2024. (Calciomercato)

Everton, West Ham na Newcastle wanatazamiwa kumkosa Federico Gatti, 26, huku mlinzi huyo wa Italia akiwa tayari kuweka hatima yake kwa Juventus. (Tuttospor)

Winga Mfaransa Allan Saint-Maximin, mwenye umri wa miaka 27, anatarajiwa kuondoka Al-Ahli ili kuungana na Jose Mourinho huko katika klabu ya Fenerbahce. (Yagız Sabuncuoglu)

Arsenal, Manchester United na Aston Villa wanamuwania winga wa Girona na Ukraine Viktor Tsygankov, 26. (AS )

Nottingham Forest wameanza mazungumzo na Fiorentina kwa ajili ya kumnunua beki wa Serbia Nikola Milenkovic, 26. (Gianluca di Marzio)

Leicester wako tayari kutoa £21.5m kwa mshambuliaji wa Juventus Muajentina Matias Soule, 21. (La Gazzetta dello Sport )
Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 14 Julai, 2024 Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 14 Julai, 2024 Reviewed by Zero Degree on 7/14/2024 08:41:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.