Loading...

VIRUSI HATARI KWA VIUMBE VYAGUNDULIWA.

virusi vinawashambulia zaidi viumbe hawa

Watafiti wa masuala ya viume vya ardhini na majini, wamegundua virusi vipya vinavyoangamiza kizazi kizazi hicho kusini mwa nchi ya Hispania.
Wahafidhina wa mambo ya viumbe wanasema kwamba virusi hivyo vinauwezo wa kurukia viumbe wakiwemo vyura,uyoga,mijusi,mijusi ya majini na kuna uwezekano nyoka pia wakaathiriwa na virusi hivyo.
Virusi hivyo vinauwezo mkubwa wa kushambulia ngozi ya tumbo la viumbe hivyo na kusababisha kansa na hufa kutokana na kuvuja damu mfululizo tumboni.
Kiongozi wa utafiti huo dokta Stephen Price kutoka katika chuo kikuu cha London anasema kwamba kuna dalili kuwa ugonjwa huo unasambaa.
Na ugonjwa huo umeshaonekana katika nchi ya China ,ufaransa na hata Netherland.
VIRUSI HATARI KWA VIUMBE VYAGUNDULIWA. VIRUSI HATARI KWA VIUMBE VYAGUNDULIWA. Reviewed by Zero Degree on 10/17/2014 09:42:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.