Loading...

Rwanda: Bunge laidhinisha muhula wa 3


Bunge la chini la Rwanda limeidhinisha mabadiliko ya katiba yanayopendekeza rais Paul Kagame aendelea kutawala kwa muhula wa tatu licha ya pingamizi kutoka kwa mataifa ya Magharibi na mashirika ya kupigania demokrasia.

Wafuasi wa milioni 4 wa Kagame walikuwa wametia sahihi pendekezo la kumtaka aendelee kutawala hata baada ya kukamilika kwa muhula wake wa pili kama katiba inayopendekeza.
Kauli hiyo ya bunge sasa itamruhusu Kagame kuwania awamu nyengine ya miaka 7 .
Bunge la juu la seneti linatarajiwa kuidhinisha mswada huo na kutoa ithibati kufanyike kura ya maoni.
Hata hivyo uchaguzi utafanyika baada ya kukamilika kwa kipindi cha sasa mwaka wa 2017.
Mapendekezo mengine yaliyoidhinishwa katika mswada huo ni kupunguza miaka ya awamu moja kutoka miaka 7 hadi miaka mitano kuanzia mwaka wa 2024.
Mamilioni ya wafuasi wake wanadai kuwa baada ya kuijenga upya uchumi wa taifa hilo uliosambaratika baada ya mauaji ya kimbari ya mwaka wa 1994 hakuna sababu ya kumuondoa madarakani.
Hata hivyo wapinzani wake wanadai kuwa licha ya ufanisi mkubwa aliouleta katika taifa hilo dogo la Afrika, utawala wake ni wa kidikteta
Image captionBunge la juu la seneti linatarajiwa kuidhinisha mswada huo na kutoa ithibati kufanyike kura ya maoni.
Wachambuzi wanasema raia wengi wa Rwanda huenda wameogopa kupinga pendekezo hilo la kumuongezea muda madarakani.
Wabunge walikubaliana mwezi Julai kufanyia marekebisho katiba ya nchi hiyo na kuandaa kura ya maamuzi kuhusu suala hilo.
"Kuwanyima watu uhuru wa kuamua jinsi watatawaliwa si demokrasia, ni kinyume cha demokrasia,” jaji huyo amesema.
Rais Kagame ameongoza kwa mihula miwili ya miaka saba baada ya kushinda uchaguzi 2003 na 2010.
Aliingia mamlakani baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa rais wakati huo Pasteur Bizimungu.
Taifa jirani la Burundi lilikumbwa na mgogoro mnamo mwezi Aprili baada ya rais Pierre Nkurunziza kuwania uhula wa tatu .

Source: BBC
Rwanda: Bunge laidhinisha muhula wa 3 Rwanda: Bunge laidhinisha muhula wa 3 Reviewed by Zero Degree on 10/28/2015 10:30:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.