Loading...

Sudan Kusini walibaka na kula watu:AU


Muungano wa Afrika umeilaumu jeshi la serikali ya Sudan Kusini na vikosi vya waasi kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu na uhalifu wa kivita.

Uchunguzi wa AU ulibaini kuwa mapigano yaliyotokea mwezi Disemba mwaka 2013 yalitokana na mzozo kati ya makabila ya Dinka na Nuer ndani ya kikosi cha kumlinda rais.
Aidha uchunguzi huo umebaini kuwa vikosi hivyo hasimu viliwachinja watu na kuwalazimisha watu waliodhaniwa kuwa mahasimu wao kula nyama ya binadamu na kunywa damu yao.
Image copyrightbbc
Image captionUchunguzi huo umebaini kuwa vikosi hivyo hasimu viliwachinja watu na kuwalazimisha watu waliodhaniwa kuwa mahasimu wao kula nyama ya binadamu na kunywa damu yao.
Jopo hilo la uchunguzi chini ya aliyekuwa rais wa Nigeria Olusegun Obasanjo limepata majina ya watu wanaodhaniwa kuwa walioendesha kampeini hizo za ubakaji wa wanawake na ulaji wa watu.
Ripoti hiyo imeorodhesha matukio ya utekaji na udhalilishwaji wa wanawake.
Aidha majina ya watu waliotekeleza matukio hayo imebainika kuwa ni ya raia ambao hawakuwa wakishiriki vita vyenyewe.
Image copyrightBBC World Service
Image captionMatukio mabaya zaidi yaliripotiwa katika miji ya Juba, Bor, Bentiu na Malakal.
Matukio mabaya zaidi yaliripotiwa katika miji ya Juba, Bor, Bentiu na Malakal.
Watu kadhaa walioshuhudia mwanzo wa vita hivyo mjini Juba wanasema kuwa walilazimishwa kunywa damu ya watu ambao ndio walikuwa wameuawa.
Makaburi ya halaiki pia yalifichuliwa katika uchunguzi huo ulioendeshwa tangu mwaka jana jopo hilo la uchunguzi lilipoundwa.
Image copyrightReuters
Image captionMakubaliano baina ya viongozi wakuu yamekiukwa
Jopo hilo limependekeza watu waliotajwa wafikishwe katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita iliyoundwa na muungano huo wa Afrika.
Licha ya hofu ya kuwa maelfu ya watu wa kabila fulani walilengwa na kuuawa jopo hilo linasema kuwa Hakukuwa na ushahidi uliopatikana wa kuthibitisha kuwa kulifanyika mauaji ya kimbari.
Image captionMiji ya Juba, Bor, Bentiu na Malakal ndio iliyoathirika zaidi
Maelfu ya watu wameripotiwa kufariki tangu kuanza kwa vita hivyo yapata miaka miwili.
Watu zaidi ya milioni mbili wamelazimika kutoroka makwao na kuwa wakimbizi wa ndani kwa ndani.
Source: BBC
Sudan Kusini walibaka na kula watu:AU Sudan Kusini walibaka na kula watu:AU Reviewed by Zero Degree on 10/28/2015 10:32:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.