Loading...

Wasiwasi watanda Zanzibar

Image captionZanzibar
Tume ya Uchaguzi Zanzibar imeahidi kutoa matokeo zaidi ya uchaguzi mkuu kisiwani Zanzibar.

Hatua hiyo inalenga kupunguza hofu na wasiwasi uliotanda hasa baada ya machafuko kushuhudiwa huko.
Vyombo vya usalama vimewekwa katika hali ya tahadhari kutokana na hali ya sintofahamu iliyosababishwa na mgombea wa urais wa upinzani kujitangaza kuwa mshindi.
Hatua hiyo ya imelaaniwa vikali na chama tawala cha CCM kilichotoa shinikizo kwa tume ya uchaguzi kuchukua hatua kali dhidi yake.
Image captionWasiwasi watanda Zanzibar
Mwandishi wetu, aliyeko huko anasema kuwa taharuki imetanda huko.
Maduka mengi yamesalia kuwa yamefungwa huku biashara ya kawaida na utalii ukiathirika.
Askari waliojihami wangali wamepiga doria mitaani
Zanzibar ina jumla ya wapiga kura 503,860 waliojiandikisha kupiga kura, kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar.

Credits: BBC
Wasiwasi watanda Zanzibar Wasiwasi watanda Zanzibar Reviewed by Zero Degree on 10/28/2015 11:43:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.