Uchaguzi2015:Matukio mbali mbali TZ
MATUKIO MBALIMBALI YA UCHAGUZI NCHINI TANZANIA
9.00am:NEC yatoa ufafanuzi kuhusu matokeo
Mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi NEC Damian Lubuva ametoa ufafanuzi juu ya ucheleweshaji wa matokeo ya rais kutoka majimbo mbalimbali akisema kuwa tume hiyo inatoa matokeo hayo kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo yote nchini..
7.00am:Washerehekea Kinondoni
Kulikuwa na sherehe katika jimbo la Kinondoni nchini Tanzania baada ya chama cha CUF kushinda katika eneo hilo.
Vijana waliokuwa wakifurahia ushindi huo waliimba na kuzunguka na bajaji wakiusifu ushindi huo na chama chao.
Hatahivyo maafisa wa polisi katika eneo hilo walifika katika eneo hilo na kuhakikisha kuwa hakuna fujo zozote zitakazotokea.
6.00am:Hali ya wasiwasi yatanda Zanzibar
Hatua hiyo inalenga kupunguza hofu na wasiwasi uliotanda hasa baada ya machafuko kushuhudiwa huko.
Vyombo vya usalama vimewekwa katika hali ya tahadhari kutokana na hali ya sintofahamu iliyosababishwa na mgombea wa urais wa upinzani kujitangaza kuwa mshindi.
Hatua hiyo ya imelaaniwa vikali na chama tawala cha CCM kilichotoa shinikizo kwa tume ya uchaguzi kuchukua hatua kali dhidi yake.
UMEAMKAJE?
Matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Tanzania yanaendelea kutolewa huku BBC ikiendelea kukufahamisha kuhusu matukio tofauti nchini humo. Tume ya Taifa ya Uchaguzi jana ilitangaza matokeo ya majimbo takriban 100 na matokeo zaidi yanatarajiwa leo.
Tunafuatilia pia hali ilivyo Zanzibar baada ya mtafaruku jana kuhusu kutolewa kwa matokeo ya uchaguzi. Wakati mmoja maafisa wa usalama walizingira kituo kinachotumiwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar kutangaza matokeo na hakuna aliyeruhusiwa kuingia wala kutoka. Tume ya uchaguzi humo visiwani kufikia jana jioni ilikuwa imetoa matokeo ya majimbo 31 kati ya majimbo yote 54.
Kwa habari zaidi kuhusu uchaguzi bofya Uchaguzi: #Tanzania2015
Credits: BBC
Uchaguzi2015:Matukio mbali mbali TZ
Reviewed by Zero Degree
on
10/28/2015 11:41:00 AM
Rating: