Loading...

Kanda ya ziwa yaongoza kwa kua na watu wenye ugonjwa wa mdomo sungura!!

Mwanza. Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Mwanza, Sekou - Toure, Onesmo Rwakendelya amesema mikoa ya Kanda ya Ziwa inaongoza kwa kujifungua watoto wenye ugonjwa wa mdomo sugura.

Akizungumza hospitalini hapo juzi, Dk Rwakendelya alisema kwa mwaka huzaliwa watoto wengi wenye tatizo hilo.

Alisema ugonjwa huo hutibiwa na madaktari wa upasuaji kutoka nje ya nchi kutokana na uhaba wa madaktari bingwa wanaotibu maradhi hayo hapa nchini.

“Wagonjwa hujikuta wako kwenye foleni kwa sababu madaktari wenyewe hufika nchini mara mbili tu kwa mwaka,” alisema Dk Rwakendelya.

Alisema licha ya Serikali kuanzisha chuo cha upasuaji kilichopo katika Hospitali ya KCMC Moshi, bado tatizo hilo ni kubwa, linaendelea kugharimu Serikali na wafadhili kuwaleta wataalamu kutoka nje kutoa matibabu.

“Tuna changamoto kubwa ya upungufu wa madaktari waliosomea mambo ya upasuaji wa midomo sugura, hivyo kusababisha wagonjwa wengi kupatiwa huduma hiyo wakiwa na umri mkubwa,” alisema Dk Rwakendelya.

Ofisa Habari wa Mgodi wa Buzwagi, Moses Msofe alisema sera mojawapo inayotekelezwa na mgodi huo ni ya kuimarisha sekta ya afya, hivyo kila mwaka hujitolea kuleta madaktari wanaotibu ugonjwa huo.

Msofe alisema mpaka sasa zaidi ya watu 150 wenye tatizo hilo tangu 2005 wametibiwa na mgodi huo na kwamba hivi sasa wameleta wagonjwa 50 kutoka maeneo mbalimbali kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Baadhi ya wagonjwa waliomba Serikali kuendela kutoa huduma hiyo mara kwa mara, ili kupunguza ongezeko la wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kutibiwa.

Mgonjwa mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Elizaberth Cheye alisema aliamini kuwa ugonjwa huo ni laana kutoka kwa wazazi wake au amelogwa lakini amekuja kubaini kuwa ni sawa na ugonjwa mwingine wowote na hutibika.

“Huduma tunayopewa ni nzuri, lakini tunaomba Serikali iboreshe angalau kila baada ya miezi mitatu madaktari hawa wawe wanakuja ili kupunguza ongezeko la wagonjwa,” alisema Ramadhan Simon.

HABARI NYINGINE KAMA HIYO NI YA YULE MTOTO ALIYEFICHWA NDANI KWA MUDA WA MIEZI 9 BAAADA YA KUZALIWA NA UGONJWA HOU!!!!!

Mtoto Selemani Kolineli Mushi(Miezi kumi)
Kabla ya kufanyiwa upasuaji
Picha: Ni mtoto mwingine kutoka Mbeya aliyezaliwa na ugonjwa wa mdomo sungura na kufungiwa ndani kwa muda wa 9.

Mtoto Selemani Kolineli Mushin(Miezi kumi)kutoka Kijiji cha Igundu Kata ya Sangambi Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya amerejea salama Kijijini baada ya kufanyiwa upasuaji kutokana na kuzaliwa na matatizo ya mdomo sungura.

Mtoto huyo alifichwa ndani baada ya kuzaliwa na kutakiwa kurudi Hospitali ya Wilaya ya Chunya miezi sita baadaye lakini Baba Mzazi wa mtoto huyo aitwae Kolineli Mushin akikataa kumpeleka Hospitali akidai huo ni mpango wa Mungu.

Mwanzoni mwa mwezi Mei 2014 baada ya mtoto huyo kukutwa na mwandishi wa Mbeya yetu na kuwashauri wazazi wa mtoto ndipo walipokubali kumpeleka Hospitali ambapo dhamana hiyo ilichukuliwa na Afisa Ustawi wa jamii Anna Geleta la kusafirishwa hadi Hospitali ya CCBRT.

Selemani baada ya kupokelewa katika Hospitali ya CCBRT alifanyiwa upasuaji na kurekebishwa mdomo ambao ulikuwa ukimpa shida wakati wa kula na kupumua kwa shida na aliruhusiwa kutoka Hospitali Mei 15 Mwaka huu na kurejea Mbeya Mei 17 ambapo gharama za safari ya kwenda na kurudi na matibabu kugharamiwa na CCBRT.







More Comments & Shares this story!!! 
Kanda ya ziwa yaongoza kwa kua na watu wenye ugonjwa wa mdomo sungura!! Kanda ya ziwa yaongoza kwa kua na watu wenye ugonjwa wa mdomo sungura!! Reviewed by Zero Degree on 11/26/2015 05:18:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.