Loading...

KILIMANJARO: ‘KIA isiwe uchochoro wa dawa za kulevya’

Moshi. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makala ameuagiza uongozi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), kuhakikisha uwanja huo hautumiki kichochoro cha kupitisha dawa za kulevya.
Agizo hilo la Makala amelitoa siku chache baada ya Rais John Magufuli kuhutubia Bunge na kuapa kupambana na biashara hiyo haramu nchini.

Akihutubia Bunge, Rais Magufuli alisema dawa za kulevya ni janga linaloathiri zaidi vijana huku akiahidi kushughulikia tatizo hilo hususan kwa vigogo wa biashara hiyo.

“Nataka niwaagize leo kwamba mhakikishe uwanja huu hauwi njia ya wapitishaji dawa za kulevya. Kuruhusu hilo tunapoteza nguvu kazi ya taifa ambayo ni vijana,” alisema Makala.

Pia, Makala alitumia fursa hiyo kuwataka wafanyakazi wa Kampuni ya Kilimanjaro Airports Development (Kadco), kuhakikisha uwanja hautumiki kutorosha nyara za Serikali.

Kaimu Mkurugenzi wa Kadco, Bakari Murusuri, alisema kampuni hiyo imepata mafanikio makubwa ikiwamo kuongeza idadi ya ndege zinazotua uwanjani hapo.


Murusuri alisema pia, wamefanikiwa kudhibiti vitendo vya “wauza unga” kutumia uwanja huo kama njia ya kupitishia dawa za kulevya na kuimarisha ulinzi na usalama.





Source: Mwananchi
Mshirikishena mwenzako kuhusiana nahabari hii!!!
KILIMANJARO: ‘KIA isiwe uchochoro wa dawa za kulevya’ KILIMANJARO: ‘KIA isiwe uchochoro wa dawa za kulevya’ Reviewed by Zero Degree on 11/26/2015 12:28:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.