Mchakato wa kuanzisha mahakama ya mafisadi waanza!!
Dar es Salaam. Utekelezaji wa ahadi za Rais John Magufuli unazidi kushika kasi baada ya kuanza kwa mchakato wa kuanzisha mahakama maalumu ya kuwashughulikia mafisadi.
Jaji Kiongozi, Shaban Lila alisema jana kuwa tayari wadau mbalimbali wa haki
jinai wameanza kukutana kuangalia namna ya kuanzisha mahakama hiyo kama sehemu
ya utekejezaji wa ahadi ya Rais.
Akizungumza katika hafla ya kuhitimisha mafunzo ya kushughulikia mashauri
nyeti ya jinai kwa majaji 12 wa Mahakama Kuu ya Tanzania, alisema juzi walikuwa
na mazungumzo na Wizara ya Katiba na Sheria kuangalia mfumo wa uendeshaji wa
mahakama hiyo.
“Tunaangalia tuianzishe kama mahakama huru au ifanywe ndani ya muundo wetu wa
mahakama kwa kuipa kipaumbele maalumu. Lakini tunafikiria zaidi kama ingekuwa ni
kitengo maalumu ndani ya Mahakama Kuu kitakachokuwa kikishughulikia mafisadi,”
alisema Jaji Lila.
Hata hivyo, Jaji Lila hakutaja muda maalumu utakaotumika kumaliza mchakato wa
kuanzisha mahakama hiyo, huku akisema unahusisha wadau wengi na unyeti wake
unahitaji maandalizi makubwa.
Jaji huyo bila kutaja takwimu, alieleza kuwa kesi za makosa makubwa ya jinai
zinaongezeka nchini ukilinganisha na miaka ya nyuma hasa zile zinazohusu
utakatishaji fedha, ugaidi, usafirishaji wa dawa za kulevya, usafirishaji wa
nyara za Serikali hasa wanyama hai na mazao yake na ufisadi.
Balozi wa Uingereza nchini, Dianna Melrose alimpongeza Rais Magufuli kwa
kuonyesha msimamo wa kupambana na makosa ya jinai yakiwamo ya dawa ya kulevya,
usafirishaji wa nyara za Serikali na utakatishaji fedha.
“Nilikuwa nimeketi bungeni namsikiliza Rais siku alipokuwa akilihutubia
Bunge, japo hotuba yake ilikuwa kwa Kiswahili lakini nilipata faraja kubwa
nilipomuona akiwa mkali katika masuala hayo,” alisema Balozi Melrose.
Credits: Mwananchi
Mshirikishe na mwenzako kuhusu habari hii!!!!
Credits: Mwananchi
Mshirikishe na mwenzako kuhusu habari hii!!!!
Mchakato wa kuanzisha mahakama ya mafisadi waanza!!
Reviewed by Zero Degree
on
11/26/2015 12:19:00 PM
Rating: