LONDON: Eden Hazard akana uvumi wa kuwepo kwa mvutano baina yake yeye na Mourinho

Macho yote yamekuwa yakimwangazia Mourinho kufuatia matokeo duni ya mabingwa hao watetezi ambao kwa sasa wanaorodheshwa ya 15 kwenye msimamo wa ligi ya mabingwa huku ikiachwa kwa alama 14 na viongozi Leicester.
"sina tatizo lolote naye. Natumai tutashinda vikombe zaidi pamoja.'
'Huenda ikawa sio msimu huu kwani ni vigumu sana, lakini misimu ujayo." Alisema hazard aliye na umri wa miaka 24.
Blues walitwaa nafasi ya 15 iliyokuwa ikishikiliwa na Norwich baada ya kuitandika 1-0 jumamosi iliyopita.
Ushindi huo ulikuwa ushindi wao wa nne pekee katika mechi 13 walioshiriki msimu huu.
Hazard, ambaye anasemekana yuko njiani kuelekea Real Madrid ya Uhispania hajaifungia Chelsea bao lolote katika mechi 18 .

Hazard alifunga mabao 20 msimu uliopita na kuibuka mshindi wa tuzo za mwanasoka bora wa soka wa kulipwa pamoja na mwanasoka bora wa mwaka katika tuzo ya waandishi wa habari za soka.
Akizungmzia hali yake ya sasa, Hazard alisema, “sikuanza msimu huu vyema. '
''Nilijaribu kujuani kwa sababu gani, japo sikujua. Wakati mwingine hujui. Lazime utie bidii.'
'Nilitia bidii kwenye mazoezi na kwa uwanja nikicheza. 'Natumai kuregelea hali yangu ya kawaida ili nijaribu kusaidia klabu yangu kushinda mechi”
Source: BBC
Share this news to all your friends.
LONDON: Eden Hazard akana uvumi wa kuwepo kwa mvutano baina yake yeye na Mourinho
Reviewed by Zero Degree
on
11/23/2015 03:43:00 PM
Rating: