Loading...

Dar es salaam: Serikali kuongeza idadi ya watalii nchini!!!

Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Wilson

Serikali ya Tanzania kupitia ubalozi wake wa Washington DC, Marekani, imeanza mikakati ya kuongeza idadi ya watalii wanaotoka nchini humo kutoka 69,000 hadi kufikia 300,000 kwa mwaka.


Akitoa salamu za mwisho wa mwaka, Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Wilson Masilingi alisema ongezeko hilo litachangia kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta ya utalii.

Balozi Masilingi alisema kwa kushirikiana na Wizara ya Usafirishaji ya Marekani, wameanza mazungumzo na baadhi ya mashirika ya ndege ya nchini humo.

Alisema wanachokifanya kwa sasa ni kuangalia namna ya kuimarisha ushirikiano na ukaribu na mashirika ya ndege kwa kuwa hali hiyo itasaidia watalii wengi kusafiri bila vikwazo, ikiwamo gharama kubwa.

Aliwataka Watanzania wanaoishi Marekani kutumia fursa zilizopo kuendelea kuitangaza Tanzania, ili vivutio vilivyopo viendelee kujulikana.

Balozi Masilingi pia, aliwataka Watanzania wanaoishi Marekani kurejea ili kuwekeza kwenye sekta ya viwanda na biashara, kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi.

Alisema wanaunga mkono jitihada za Rais John Magufuli katika kukuza uwekezaji.



Credits: Mwananchi

Mshirikishe namwenzako kuhusu habari hii!!
Dar es salaam: Serikali kuongeza idadi ya watalii nchini!!! Dar es salaam: Serikali kuongeza idadi ya watalii nchini!!! Reviewed by Zero Degree on 12/26/2015 04:20:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.