Loading...

Mwanamke atiwa mbaroni baada ya kukutwa akifanya USHIRIKINA jikoni!!!


Mkazi mmoja wa Kijijini Lamadi wilayani Busega, Mkoa wa Simiyu anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kukutwa mtupu akijihusisha na ushirikina katika familia ya Yusta Thomas.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Gemini Mushy alisema juzi kuwa tukio hilo lilitokea saa nane usiku wa kuamkia Jumanne iliyopita.

Kamanda Mushy alisema mama wa familia hiyo alisikia sauti za watu nje wakinong’onezana, ndipo alipotoka na kumkuta mwanamke huyo akiwa jikoni amening’inia bila kujitambua.

Alisema kuona hivyo, mama huyo alipiga kelele kuomba msaada kwa majirani kwa kuwa mumewe hakuwapo.

Kamanda Mushy alisema mwanamke huyo alikataa kushuka darini hadi asubuhi walipofika askari na kumwamuru ashuke.

Alisema baada ya kuvishwa nguo waliondoka naye hadi kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi.

Kamanda Mushy alisema mtuhumiwa huyo anaendelea kufanyiwa uchunguzi na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma za kujihusha na ushirikina.

Tukio hilo la kuhusiana na imani za ushirikina ni la pili kutokea wilayani Busega. Septemba 3, 2014 katika Kata ya Kalemela watu wanne wa familia moja walikutwa asubuhi wakilima shambani wakiwa watupu.


Credits: Mwananchi


Mshirikishe na mwenzako kuhusu habari hii!!
Mwanamke atiwa mbaroni baada ya kukutwa akifanya USHIRIKINA jikoni!!! Mwanamke atiwa mbaroni baada ya kukutwa akifanya USHIRIKINA jikoni!!! Reviewed by Zero Degree on 12/26/2015 04:37:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.