Dar es Salaam: Taasisi 1,200 duniani zampa tuzo ya AMANI Mh. Edward Lowassa!!!
Akizungumza na Mwananchi kutoka Bukavu, DR Congo, mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa jamii, Mchungaji William Mwamalanga alisema Lowassa amechaguliwa jana mjini Bukavu na wajumbe 1,400 wa mkutano huo.
Mwamalanga alisema wajumbe wanaohudhuria kongamano la amani wanatoka mataifa ya Ulaya, Marekani, Asia na Afrika kwa kuwashindanisha wanasiasa 1,000 ili kumpata Kiongozi Bora wa Amani mwaka 2015, ambaye anajali na kuangalia maslahi ya jamii badala ya madaraka.
Hatua ya kumpatia tuzo Lowassa ni baada ya kuelezwa kuwa amedumisha amani hiyo hata baada ya kushindwa uchaguzi Mkuu wa Rais Oktoba 25.
Katika uchaguzi uliopita, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)ilimtangaza Dk John Magufuli kuwa mshindi kwa kupata kura 8,882,935 ikiwa ni asilimia 58.46 wakati Lowassa alipata kura 6,072,848 sawa na asilimia 39.97 ya kura zote.
Mchungaji Mwamalanga alisema katika kongamano hilo, wajumbe walijadili hali ya amani duniani na mchango wa wanasiasa katika kulinda amani hiyo.
Alisema kuwa wanasiasa barani Afrika wamekuwa vyanzo vya migogoro na mauaji ya raia wakati wa uchaguzi, kama ilivyo nchini Burundi. Hata hivyo, alisema kuwa wajumbe walipongeza ushindi wa Dk Magufuli, lakini wakasema umetiwa dosari na hali ya kisiasa Zanzibar baada ya matokeo kufutwa.
Alisema wajumbe wa kongamano hilo linaloshirikisha maaskofu, masheikh na vijana kutoka madhehebu mbalimbali ya dini barani Afrika, wamemuhimiza Rais Magufuli kumaliza utata wa uchaguzi wa Zanzibar.
Baada ya kupitishwa kugombea urais kwa tiketi ya Chadema, Lowassa alitangaza kuwa angefanya kampeni kistaarabu na kwa amani na baada ya matokeo aliwatuliza wafuasi wa chama hicho, akisema “hakuna anayeweza kuizuia bahati ya mtu” kwa hiyo kama amepangiwa kuwa rais, atakuwa.
Lowassa, ambaye ni Waziri Mkuu wa kwanza wa Serikali ya Awamu ya Nne, aliongeza upinzani kwenye uchaguzi wa mwaka huu baada ya kuihama CCM na kujiunga na Chadema iliyoukuwa na nguvu ya vyama vingine vitatu vya NLD, CUF na NCCR-Mageuzi.
Kama alivyoahidi, Lowassa hakutumia mikutano yake ya kampeni kushambulia mabo binafsi ya wagombea wengine, bali muda mfupi kuomba kura.
Credits:Mwananchi
Mshrikishe na mwenzako kuhusu habari hii!!
Dar es Salaam: Taasisi 1,200 duniani zampa tuzo ya AMANI Mh. Edward Lowassa!!!
Reviewed by Zero Degree
on
12/19/2015 02:46:00 PM
Rating: