Dawasco yapandisha bei ya maji!!
Dar es Salaam. Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasco), limeanza rasmi kutumia bei mpya za ankara za maji, ikiwa ni siku chache baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji (Ewura) kupitisha mapendekezo ya kupandisha bei kama walivyoomba.
Awali, Dawasco iliomba kuongeza bei ya utoaji wa huduma hiyo ili kuboresha huduma zake katika Jiji la Dar es Salaam, Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani.
Bei hizo mpya ambazo zimeanza rasmi kutumika Desemba Mosi, zimepanda kutoka kiasi cha Sh1,098 kwa lita 1,000 hadi kufikia Sh1,663 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 51.
Ofisa Habari wa Dawasco, Everlisting Lyaro alisema kupitishwa kwa mapendekezo hayo kutaongeza uwezo wa shirika hilo kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo kwa wateja wao.
“Lakini pia huduma zitaboreshwa zaidi baada ya kukamilisha miradi yote mikubwa ya maji ambayo tayari ipo katika hatua zake za mwisho,” alisema Eva.
Wakazi wa jijini Dar es salaam, wameiomba Dawasco kuhakikisha inawapatia huduma hiyo kulingana na mahitaji yao huku ikiendana na gharama iliyoongezwa.
“Sisi hatuna shida na ongezeko la bei, tunachotaka ni huduma bora ya maji, Dawasco wahakikishe wananchi tunapata huduma hiyo bila usumbufu, siyo wanaongeza bei halafu maji yenyewe hatuyapati, hapo hatutakubali kabisa,” alisema Penieli Tenga, mkazi wa Mwananyamala Manispaa ya Kinondoni.

Credits: Mwananchi
Mshirikishe na mwenzako kuhusiana na habari hii!!
Dawasco yapandisha bei ya maji!!
Reviewed by Zero Degree
on
12/06/2015 11:26:00 AM
Rating: