Dar es salaam: Hospitali ya Amana sasa yaanza kutoa huduma kwa njia ya mtandao!!!
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Meshack Shimwela akizungumza na waandishi wa habari. Ili kudhibiti upotevu wa mapato na kuboresha huduma, Hospitali ya Wilaya ya Ilala Amana, imeanza kutoa huduma zake kwa njia ya mtandao kuanzia kujisajili hadi mgonjwa anapolipia gharama za matibabu.
Akizungumzia utaratibu huo, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Meshack Shimwela alisema teknolojia hiyo imeisaidia hospitali kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato na kusimamia huduma kwa karibu kati ya mgonjwa na watoa huduma.
Alisema mgonjwa yeyote hivi sasa haruhusiwi kumkabidhi fedha taslimu muhudumu wa hospitali bali mpokea malipo ambaye huichanja kadi yake kuonyesha kuwa amelipa fedha halali aliyotozwa kwa matibabu.
Mwananchi lililofika hospitalini hapo na kuzungumza na baadhi ya wagonjwa ambao walionyesha kufurahishwa na utaratibu huo.
Walisema umesaidia pia kupunguza foleni hospitalini hapo.
Mmoja wa wagonjwa waliofika kutibiwa katika hospitali hiyo, Yeledi Livingstone, alisema huduma hiyo imesaidia mgonjwa kupata matibabu kwa haraka tofauti na awali.
Mgonjwa mwingine ambaye hakutaka kutajwa jina gazetini, alisema lifika hospitalini hapo kwa ajili ya vipimo na kupiga picha X - Ray, na alitakiwa kulipa gharama ya Sh3,000, aliilipa kwa kutumia kadi yake ya benki.
“Jana nilikuwa sijaingiziwa fedha ofisini, zikaingizwa jioni ndiyo maana nimekuja leo nimelipa kwa kadi yangu ya benki na nimefika dirishani nikajieleza taarifa zangu zikatumwa huku imefika zamu yangu nimeitwa kwenda kumuona daktari kwa matibabu zaidi,” alisema.
Mgonjwa mwingine, Zamda Athumani alisema:
“Hii narudi mara ya pili, wasipoingiza taarifa vizuri utaganda kwa daktari, kwenye vipimo na ukiuliza wahusika wakikuangalia kama haupo hupati huduma, nimerudi wamerekebisha ndiyo nakwenda kumuona daktari sasa,” alisema Zamda.
Credits:Mwananchi
Mshirikishe na mwengine kusiana na habari hii!!!
Dar es salaam: Hospitali ya Amana sasa yaanza kutoa huduma kwa njia ya mtandao!!!
Reviewed by Zero Degree
on
12/06/2015 11:34:00 AM
Rating: