KIAMA: Mvua kali iliyonyesha Arusha yaua watu watatu, na kusababisha kaya zaidi ya 70 kukosa makazi!!!
Mvua ilinyesha jana ikiwa ni siku ya tatu mfululizo, imesababisha adha kwa mabondeni katika kata nane za Halmashauri ya Arusha Vijijini wilayani Arumeru.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha vijijini, Fidelis Lumato alizitaja kata hizo kuwa ni ya Ortumet, Lemanyata, Orkokola, Muandeti, Mussa, Oljoro, Oldonyosambu na Kisongo.
Alisema ng’ombe zaidi ya 20, kuku 120, na kondoo 40 wamekufa kwa kusombwa na maji.
“Ingawa hatuna majina ya watu waliopoteza maisha, lakini mmoja anatoka Kata ya Ortumet na wawili Kata ya Muandet. Kamati ya maafa imekaa kikao na mkuu wa wilaya pamoja na maofisa wa Tanroad ili kubaini chanzo cha maji hayo kuelekea zaidi kwenye makazi ya watu,” alisema.
Wakizungumzia mafuriko hayo, baadhi ya wakazi wa Ngaramtoni walidai kuwa chanzo ni mitaro ya Barabara ya Arusha-Namanga ambayo mitaro yake imeelekezwa kwenye makazi ya watu.
Barabara hiyo ni miongoni mwa zile zilizozinduliwa na viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki 2012, ikiwa na urefu wa kilomita 104 kwa upande wa Tanzania.
Hata hivyo, Mkurugenzi Lumato alisema kuwa ujenzi wa mtaro huo utaanza mara moja ili kunusuru makazi ya watu na utaanzia katika eneo la Lengijaphe na kuelekezwa eneo la Orkurot yaliko machimbo ya moram.
Alitoa wito pia kwa wakazi wanaoishi mabondeni kuhama mara moja ili kuepuka maafa zaidi wakati wa mvua za masika.
Credits: Mwananchi
Mshirikishe na mwenzako kuhusu habari hii!!
KIAMA: Mvua kali iliyonyesha Arusha yaua watu watatu, na kusababisha kaya zaidi ya 70 kukosa makazi!!!
Reviewed by Zero Degree
on
12/17/2015 10:25:00 AM
Rating: