Loading...

Ajinyonga akidai siku za kuishi zimekwisha.


Katavi. Mkazi wa Kijiji Cha Igagala Wilaya ya Mpanda, Juma Sadi (50) amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kamba ya chandarua kwa madai kuwa dawa za kienyeji alizokunywa kumzuia asife mapema zilikwisha nguvu.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Igagala, Athumani Juma alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 5:30 usiku jirani na nyumba aliyokuwa akiishi.

Juma alisema kabla ya tukio hilo, Sadi alimweleza shemeji yake kuwa lazima afe kwa kuwa alimeza dawa za kienyeji (mpigi) vipande vitatu ili asife mapema lakini amevitapika viwili hivyo hana kinga tena.

Hata hivyo, alisema shemeji yake alimpuuza hali iliyomfanya Sadi aondoke eneo hilo hadi nyumbani kwake na kumwambia mkewe ampikie uji ili anywe.

Juma alisema muda mfupi baadaye, Sadi alimuaga mkewe kuwa anakwenda kufungia mbuzi huku akiwa na kamba ya chandarua. Alisema hakurejea ndani hadi majirani walipomwona akining’inia juu ya mti wa mwembe uliokuwa jirani na nyumba yake.



ZeroDegreee.
Ajinyonga akidai siku za kuishi zimekwisha. Ajinyonga akidai siku za kuishi zimekwisha. Reviewed by Zero Degree on 1/20/2016 03:45:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.