Loading...

ALIYETAPELI millioni 600 kwa UGANGA anaswa.

Kamanda wa polisi wa mkoa Kilimanjaro ,
Kamanda wa polisi wa mkoa Kilimanjaro , Ramadhan Mungi.
Moshi. Jeshi la Polisi limefanikiwa kumtia mbaroni mkazi mmoja wa jijini Dar es Salaam, anayetuhumiwa kujifanya mganga wa kienyeji na kumtapeli mke wa mmiliki wa shule moja ya sekondari Sh600 milioni.


Mtuhumiwa huyo alifanikiwa kutapeli fedha hizo baada ya mwanamke huyo kukataa ushauri wa awali kuwa ili dawa ya kufanya wanafunzi wafurike shuleni hapo ifanye kazi, waue mwanafunzi mmoja kimazingara. Alipokataa ushauri huo ndipo alipoambiwa atoe fedha ili atengenezewe dawa mbadala.

“Yuko hapo kituo kikuu cha Mkoa wa Kilimanjaro. Mimi nilimuuliza ilikuwaje akasema ni kweli alichukua fedha hizo lakini kwa makubaliano ya uganga. Inaonekana kuna zaidi ya uganga,” alidokeza polisi mmoja.

Kamanda wa polisi wa mkoa, Ramadhan Mungi aliomba apewe muda hadi leo atakapotoa taarifa sahihi, lakini wiki iliyopita aliyekuwa kaimu kamanda wa mkoa, Koka Moita alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo.



Source:Mwananchi


Comment & Share this story!!
ALIYETAPELI millioni 600 kwa UGANGA anaswa. ALIYETAPELI millioni 600 kwa UGANGA anaswa. Reviewed by Zero Degree on 1/04/2016 02:57:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.