Loading...

ANC yaichagua Tanzania kuwa shule yake ya siasa.


Katibu Mkuu wa ANC, Gwede Mantase

Dar es Salaam. Chama cha African National Congress (ANC) cha Afrika Kusini, kimeitangaza Tanzania kuwa shule yake ya siasa kikanda.

Imeelezwa kuwa, Tanzania imepewa kipaumbele na chama hicho kutokana na mchango mkubwa iliyoutoa wakati wa harakati zake za ukombozi wa Kusini mwa Afrika.

Katibu Mkuu wa ANC, Gwede Mantase amesema leo kuwa, changamoto kama ya uwapo wa makundi, rushwa na upendeleo ndani ya chama hicho, kunatokana na ukosefu wa elimu ya siasa.

Chama hicho tawala, kiliamua tangu 2007 kuwa wajumbe wote wa kamati kuu taifa, wapate mafunzo kutoka shule ya siasa ili kuondoa changamoto zinazoweza kukikabili.

Mantase amesema tatizo la kukosa elimu ya siasa, linavikabili vyama vingi vya ukombozi vinavyoongoza nchi kadhaa barani Afrika.

“Hilo siyo tatizo la Waafrika Kusini pekee, bali ni la vyama vyote vya ukombozi Afrika. Sisi ni viongozi wa vyama, tukiwa miongoni mwa walio kwenye historia hiyo, tunatakiwa kuleta mabadiliko, lazima tuwape mafunzo wanachama wetu wapya wasio na uelewa juu ya historia ya chama na pia ya safari ya harakati za ukombozi,” amesema.

Amesema, chanzo cha kuichagua Tanzania kuwa chuo cha siasa ni baada ya kukubali kuwapokea wanachama kadhaa wa ANC waliowahi kutumikia kifungo wakati wa mapambano ya ukombozi.

“Hilo ni jambo lililochangia kuichagua kuwa eneo litakalotumika kwa ajili ya shule hiyo,” amesema Mantase.

Amesema mradi wa mafunzo hayo utafadhiliwa na Chama cha Kikomunist cha China. Kwa upande wa Afrika Kusini, shule ya siasa itajengwa katika eneo la Potchefstroom, Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo na mradi utafadhiliwa na Jiji la Beijing.



Source: Mwananchi
ANC yaichagua Tanzania kuwa shule yake ya siasa.  ANC yaichagua Tanzania kuwa shule yake ya siasa. Reviewed by Zero Degree on 1/13/2016 01:08:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.