Dk Shein ashiriki katika shughuli za usafi wa soko la matunda Zanzibar.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kushiriki kazi ya kufanya usafi katika soko la matunda la Mombasa mjini Unguja jana, alisema wananchi wanaelewa vyema historia ya Mapinduzi ya Zanzibar na kwamba, wanatambua wajibu wao katika kuyalinda na kuyadumisha.
Dk Shein alisisitiza kuwa, kila mtu ana haki na wajibu wa kuyaenzi na kuyaendeleza Mapinduzi ya 1964 kwa sababu mapaka sasa hakuna mtu hata mmoja visiwani humo asiyethamini uhuru wake.
Alisema Mapinduzi hayo yalifanyika kwa malengo maalumu ya kuwakomboa Wazanzibari kutoka katika mazingira yaliyokuwapo wakati huo.
Hata hivyo, alisema wapo baadhi ya watu wanaoyakumbuka kwa furaha na wengine wananuna.
Aliwataka wananchi kushiriki kikamilifu katika kila hatua ya maadhimisho hayo.
Source: Mwananchi
Commment & Share this story!!
Dk Shein ashiriki katika shughuli za usafi wa soko la matunda Zanzibar.
Reviewed by Zero Degree
on
1/04/2016 03:14:00 PM
Rating: