Edward Lowassa na Waziri mkuu Kasimu Majaliwa kuhudhuria tukio la kuingizwa kazini kwa Mkuu mpya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk Fredrick Shoo.
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.
Moshi. Maaskofu zaidi ya 30 kutoka ndani na nje ya nchi, leo wanatarajiwa kuhudhuria tukio la kuingizwa kazini kwa Mkuu mpya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk Fredrick Shoo.
Miongoni mwa maaskofu hao ni pamoja na 24 wa dayosisi zote za KKKT, maaskofu wa lutherani kutoka mataifa mbalimbali duniani na maaskofu wa makanisa rafiki.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tukio hilo litakalofanyika katika Usharika wa Moshi na aliwasili mjini hapa jana.
Pia tukio hilo litashuhudiwa na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, wabunge na viongozi mbalimbali wa Serikali.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ambaye pia ni Mkuu wa Pili wa Jimbo Kilimanjaro Kati la KKKT, Mchungaji Fred Njama aliliambia gazeti hili kuwa, viongozi mbalimbali wamethibitisha kushiriki.
Kulingana na ratiba iliyotolewa, Dk Shoo ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini ataingizwa kazini katika ibada itakayoendeshwa na Mkuu wa KKKT mstaafu, Dk Alex Malasusa.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makala aliwaambia waandishi wa habari juzi kuwa, Majaliwa angewasili na tukio linalomleta ni la sherehe hizo.
Dk Shoo alichaguliwa kuwa mkuu wa kanisa hilo katika mkutano mkuu wa 19 wa KKKT uliofanyika Agosti 14, mwaka jana na atatumikia wadhifa huo kwa kipindi cha miaka minne.
Katika mkutano wa uchaguzi askofu huyo alipata kura 153 dhidi ya 67 za Askofu Dk Stephen Munga wa Dayosisi ya Kaskazini ambaye alichuana naye katika duru ya pili.
ZeroDegree.
Edward Lowassa na Waziri mkuu Kasimu Majaliwa kuhudhuria tukio la kuingizwa kazini kwa Mkuu mpya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk Fredrick Shoo.
Reviewed by Zero Degree
on
1/31/2016 04:13:00 PM
Rating: