Loading...

Jalada la kesi ya mauaji [ ya mwaka 2009 ] ya matajiri wanne ndugu wa familia moja Mwanza, latinga kwa (DPP).


Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Biswalo Mganga .

Dar es Salaam. Jalada la kesi ya mauaji yanayodaiwa kufanywa mwaka 2009 na matajiri wanne wa Mwanza ambao ni ndugu wa familia moja, limepelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) jijini Dar ss Salaam kwa ajili ya hatua za kisheria.

Hata hivyo, tangu jalada hilo lipelekwe kwa DPP Januari 20, bado ofisi hiyo haijatoa mwongozo wa kisheria endapo kesi hiyo sasa ifunguliwe rasmi katika mahakama ya makimu mkazi mjini Moshi.

Ni kutokana na kuchelewa kutolewa kwa ushauri huo wa kisheria, watuhumiwa watatu ambao walitiwa mbaroni jijini Mwanza wiki tatu zilizopita, wanaendelea kusota polisi bila kufunguliwa mashitaka.

“Ulizeni ofisi ya DPP mkituuliza sisi polisi kwa nini hawajafikishwa mahakamani hadi leo, mnatuonea. Jalada lilipelekwa kwa DPP tangu Jumatano iliyopita,”alisema ofisa mmoja wa Jeshi la Polisi.

Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Biswalo Mganga aliwataka wahusika kuwa wavumilivu kwa maelezo kuwa ofisi yake inafanya kazi kwa kufuata utaratibu na kwa mujibu wa sheria.

“Siwezi kutoa majibu kwenye magazeti. Tunafanya kazi kwa kufuata utaratibu na jalada hili likikamilika basi watajulishwa,” alisema.

Habari zinadai kuwa ili kuirahisishia ofisi ya DPP kulipitia jalada hilo kwa uharaka, ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ilipeleka jalada hilo likiwa na maelezo halisi na yale yaliyochapwa kwa mashine.

Kukamatwa kwa matajiri hao wawili kati ya wanne wanaotuhumiwa kufanya mauaji hayo, kulitokana na barua ya ndugu wa marehemu waliyomwandikia Rais John Magufuli kulalamika kutokamatwa kwao.

Baada ya barua hiyo, DCI aliteua kikosi kazi chini ya Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Charles Kenyela akisaidiwa na Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Ralph Meela, kufanya uchunguzi upya.

Ni kutokana na uchunguzi wa kikosi hicho, polisi lifanikiwa kupata ushahidi kutoka kwa watu 16 ambao ni pamoja na walioshuhudia mauaji hayo na ndugu wa karibu wa marehemu.

 Wafanyabiashara wanatuhumiwa kumteka meneja wa baa ya Mo-Town, James Massawe na kwenda kumuua kwa mateso nyumbani kwao eneo la Kibosho.

Miongoni mwa walioandikisha upya maelezo yao, ni vijana watatu waliokuwa wakiteswa pamoja na marehemu, ambao ushahidi wao pamoja na wengine waliuoshuhudia unategemewa kuwa msingi wa kesi. 

Wiki mbili zilizopita, DCI Diwani Athman alikataa kuzungumzia kwa undani kuhusu suala hilo, akisema liko kwenye uchunguzi na kama atafanya hivyo anaweza kuingilia uchunguzi unaoendelea.



ZeroDegree.
Jalada la kesi ya mauaji [ ya mwaka 2009 ] ya matajiri wanne ndugu wa familia moja Mwanza, latinga kwa (DPP). Jalada la kesi ya mauaji  [ ya mwaka 2009 ] ya matajiri wanne ndugu wa familia moja Mwanza, latinga kwa (DPP). Reviewed by Zero Degree on 1/31/2016 04:22:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.