Kigoma wafurahia ziara ya Waziri mkuu.
Mbunge wa Kakonko, Kasuku Bilago alisema kitendo cha Waziri mkuu kuwabana watendaji na kutaka kila mmoja atimize wajibu wake, kitasaidia kuondoa ukiritimba uliokuwa umekithiri miongoni mwao.
Alisema baadhi ya maofisa wa Serikali huwatolea kauli zisizofaa wananchi wanaokwenda kuhijitaji huduma kwenye ofisi zao.
“Kitendo cha kuwaambia atakayebainika kufanya hivyo ajiandae kufungasha virago, kitawafanya waache kufanya kazi kwa mazoea,” alisema.
Muuguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Maweni ya Mkoa wa Kigoma aliyekataa kuandikwa jina gazetini, alisema; “Baadhi yetu hatujitumi kufanya kazi yetu kwa mujibu wa utaratibu, lakini hii yote ilisababishwa na viongozi kushindwa kusimamia mfumo wa utendaji kazi.
“Kila siku wagonjwa wanalalamikia huduma mbovu zinazotolewa katika hospitali nyingi za Serikali, lakini siyo kwamba watu hawawezi kufanya kazi, hapana, wanaiga kile kinachofanywa na viongozi,” alisema muuguzi huyo.
Mkazi wa Katubuka, Josia Gabriel alisema ujio wa Waziri Mkuu, Majaliwa utaleta ufanisi katika Manispaa ya Kigoma Ujiji ambayo ilikuwa ikilalamikiwa na wananchi kwa ubadhirifu katika ugawaji wa viwanja.
Katika ziara hiyo, Majaliwa aliwataka wakazi mkoani Kigoma kutoa taarifa kwa viongozi wa juu wanapobaini mtumishi anakiuka utaratibu wa kazi yake.
Alisema Serikali haitasita kumfukuza kazi yeyote atakayekiuka utaratibu wa utumishi wa umma.
Source: Mwananchi
Comment & Share this!!
Kigoma wafurahia ziara ya Waziri mkuu.
Reviewed by Zero Degree
on
1/09/2016 05:09:00 PM
Rating: