Mabaharia Watinga Wizara ya Uchukuzi Kudai Mikataba.
Wanajumuiya hiyo walivyojikusanya katika eneo hilo.
Wanajumuiya ya Mabaharia wakiwa wamesimama ndani ya geti la Wizara ya Uchukuzi jijini Dar, leo.
Mmoja wa wanajumuiya hiyo akihojiwa na wanahabari wizarani hapo.
Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mabaharia Tanzania, Ally Mohammed (aliyesimama mbele) akiwa sambamba na wenzake.
Baadhi ya wanahabari wakichukua tukio hilo.
JUMUIYA ya mabaharia hapa nchini, leo mapema wamekusanyika Makao Makuu ya Wizara ya Uchukuzi wakidai kupewa mikataba ya ajira pamoja na kuboreshewa maslahi yao.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, makamu mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Ally Mohammed, amesema kuwa lengo lao kubwa ni kutaka kupewa mikataba na posho, hivyo wanataka kuonana na waziri wa uchukuzi na kushinikiza wageni kutoka nje ya nchi kupewa kipaumbele cha kupatiwa ajira kuliko wazawa.
Naye mmoja wa wanajumuiya hiyo, alipohojiwa na wanahabari na kuulizwa ni kwa nini wasingeendelea na kazi kuliko kukusanyika wizarani hapo, alisema wanalazimika kukusanyika hapo ili kupata ukweli wa tatizo lao na si kungojea majibu kutoka kwa viongozi wao kwani wanahitaji kujiridhisha zaidi.
Wakati huohuo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, amesema kuwa anazo taarifa za uwepo wa mabaharia hao na tayari amekwishafanya vikao viwili na viongozi wao, hivyo malalamiko yao ni ya msingi na serikali tayari inayafanyia kazi.
Source: GPL
Mabaharia Watinga Wizara ya Uchukuzi Kudai Mikataba.
Reviewed by Zero Degree
on
1/15/2016 06:16:00 PM
Rating: