Saluni za NGONO Dar, kimenuka!!!
Muhudumu mmoja wa saruni akijificha kuikimbia kamera |
Mchunguzi mmoja alifanikiwa kufika ndani ya saluni iliyopo Sinza Palestina, Dar na kuulizia kama anaweza kupata huduma ya kuchuliwa ‘masaji’ na ya ngono:
“Unaweza anko. Hapa huduma zote zipo. Ni wewe tu! Lakini huduma ya masaji, unalipia elfu sitini (60,000) mapokezi, huduma ya ngono unanilipa mimi chumbani. Kazi kwako anko,” alisema mhudumu aliyekutwa.
WANAFANANA
Majibu ya mhudumu huyo hayakutofautiana na ya wahudumu wengine wanaotoa huduma ya masaji katika saluni nyingine zilizopo Mlimani City, Mikocheni na Makumbusho ambao walisema malipo ya huduma ya ngono yanafanywa chumbani kabla ya makasheshe.
MAZINGIRA YAKE
Katika masaji zote hizo, eneo la mapokezi kuna baa ndogo zilizosheheni pombe kali na vinywaji laini kwa ajili ya wateja wanaosubiri huduma au walio vyumbani wakihudumiwa.
TAMKO LA SERIKALI
Baada ya kushuhudia hayo, alitafutwa Afisa Biashara wa Manispaa ya Kinondoni, Zahoro Rashid na kutaka kujua sheria zinasemaje kuhusu usajili wa saluni hizo.
Afisa huyo alikiri kusikia fununu kuwa, baadhi ya saluni, Dar zimekuwa madanguro.
Zahoro akaweka wazi sheria ya usajili wa saluni hizo kuwa ni marufuku kuuza pombe ndani kwani leseni zao haziruhusu kileo chochote. Akawaomba waandishi kuwafichua wenye saluni ambao wanavunja maagizo hayo.
“Tunawaomba sana nyinyi waandishi mtusaidie kuzifichua hizo saluni ili tuzichukulie hatua husika ikiwemo kuzifutia leseni za biashara na kuwapeleka mahakamani,” alisema afisa huyo.
HUDUMA YA NGONO
Baada ya hapo, afisa huyo aliambiwa kuwa, kuna picha zilipigwa mwishoni mwa mwaka jana baada ya kumnasa mhudumu na mteja wakiivunja amri ya sita ya Mungu ndani ya saluni moja iliyopo Mlimani City. Sikia tamko la afisa huyo.
“Loo! Hilo ndiyo baya zaidi kuliko yote. Tena nawashukuru sana jamani. Ni kinyume cha sheria za usajili wa saluni za masaji kwa wahudumu kugeuza eneo hilo kuwa la kufanyia ngono.
“Serikali ya sasa ipo sambamba nao, wajue kwamba, kama walizoea tabia hiyo, sasa kimenuka!"
Source: GPL
Saluni za NGONO Dar, kimenuka!!!
Reviewed by Zero Degree
on
1/15/2016 06:05:00 PM
Rating: