Loading...

Makamu wa Rais awaagiza Mawakala wa Misitu (TFS), kuacha kuhamisha watu.


Geita. Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu amewaagiza Wakala wa Misitu (TFS) Mkoa wa Geita, kusimamisha mara moja kazi ya kuwahamisha watu wanaodaiwa kuvamia maeneo ya hifadhi ya msitu mkoani hapa.

Samia alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza na wakazi wa mkoani hapa, alipokuwa akihitimisha ziara yake ya siku moja.

Alisema Serikali iliagiza wizara zinazohusika kubomoa nyumba zilizojengwa katika maeneo hatarishi na yale yaliyovamiwa, lakini TFS imekiuka agizo hilo.

Aliwataka kusimamisha kazi hiyo mpaka hapo Serikali itakapotangaza vinginevyo.

Samia aliyasema hayo baada ya kupokea malalamiko ya wananchi kupitia Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma aliyedai kuwa TFS imekuwa ikiwafukuza wananchi kwenye vijiji vyao kwa madai kuwa ni maeneo ya hifadhi ya misitu.

Kwa upande mwingine Msukuma aliiomba Serikali kutimiza ahadi aliyoitoa Rais John Magufuli kwa wakazi wa Geita ya kuwapatia maeneo wachimbaji wadogo.


Source:Mwananchi

Comment & Share this!!
Makamu wa Rais awaagiza Mawakala wa Misitu (TFS), kuacha kuhamisha watu. Makamu wa Rais awaagiza Mawakala wa Misitu (TFS), kuacha kuhamisha watu. Reviewed by Zero Degree on 1/07/2016 04:27:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.