Kipindupindu chaibuka Ukerewe, chanzo kikihofiwa kuwa ni baada ya mafuriko.
Ni baada ya ugonjwa huo kuibuka upya kwa kasi wilayani hapa na kusababisha vifo vya watu wawili, huku wengine saba wakilazwa hospitali ya Wilaya mjini Nansio kwa matibabu.
Akizungumza kabla ya kikao hicho, Dk Kilasala alisema ugonjwa huo umelipuka katika maeneo ya Nansio yaliyokumbwa na mafuriko hivi karibuni.
“Maeneo ya Kata ya Nakatungulu na kitongoji cha Namagubo yameathiriwa zaidi na mafuriko, zaidi ya nyumba 134 zimebomoka na vyanzo vya maji karibu vingi hasa visima, vilifunikwa na maji,” alisema.
Hata hivyo, alisema baada ya mafuriko kupungua, watu waliendelea kuyatumia maji hayo ya visima, hali inayodaiwa huenda kikawa chanzo cha kipindupindu,” alisema Dk Kilasala.
Alitoa wito kwa wakazi wa maeneo hayo, kuzingatia kanuni za afya kwa kuhakikisha wanachemsha maji ya kunywa, kunawa mikono kwa maji safi na sabuni kabla ya kula chakula na baada ya kutoka msalani ili kuepuka kuenea zaidi kwa ugonjwa huoa.
Mlipuko wa kipindupindu uliikumba Ukerewe tangu Septemba mwaka jana na kuwakumbuka zaidi ya watu 250, kati yao 13 walikufa kabla ya kudhibitiwa.
Hata hivyo, Dk Kilasala alisema katika kukabiliana na ugonjwa huo, tayari Idara ya Afya ya wilaya imepiga marufuku mikusanyiko ya watu katika misiba, sherehe, magulio na kuuza vyakula na vinywaji katika mazingira yasiyokidhi vigezo vya usafi.
Source: Mwananchi
Comment & Share this!!
Kipindupindu chaibuka Ukerewe, chanzo kikihofiwa kuwa ni baada ya mafuriko.
Reviewed by Zero Degree
on
1/07/2016 04:36:00 PM
Rating: