Daktari mmoja ahudumia wagonjwa 8,000 kwa wiki, Kishapu.
Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea zahanati hiyo jana, Dk Dolina Donald, alisema wana wauguzi watatu tu ambao wamekwenda likizo.
“Wawili wako likizo ya kawaida na mmoja amechukua likizo ya uzazi, kwa hapa niko peke yangu na ninahudumia wagonjwa takribani 8,000, kwa wiki,” alisema Dk Donald.
Alisema kuna wakati anashindwa kuamua afanye kipi kwa sababu ya kuelemewa na kazi hasa wanapofika wajawazito wanaohitaji kujifungua.
“Licha ya kuwa peke yangu, hata chumba chenyewe cha kujifungulia kina kitanda kimoja, wajawazito hufikia mahali wanajifungulia chini na kusababisha watoto kufa,” alisema.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Johanes Kimulika aliitupia lawama Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushindwa kuwapatia idadi ya watumishi walioomba.
“Tulishaiandikia wizara mahitaji yetu, lakini hawajatekeleza mpaka sasa, hali hii inaleta usumbufu kwa wananchi na hata wafanyakazi wenyewe ambao wanazidiwa na kazi,” alisema Kimulika.
Hivi karibu, Waziri wa wizara hiyo, Ummy Mwalimu, alisema wanaendelea kubaini maeneo yanayokabiliwa na upungufu mkubwa wa watendaji ili waanze kuyafanyia kazi.
Source: Mwananchi
Comment & Share this!!
Daktari mmoja ahudumia wagonjwa 8,000 kwa wiki, Kishapu.
Reviewed by Zero Degree
on
1/07/2016 04:44:00 PM
Rating: