Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) yatahadharisha mvua kubwa kuanza ndani ya siku 3 kuanzia jana.
Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetahadharisha kutokea kwa mvua kubwa ndani ya siku tatu kuanzia jana usiku hadi kesho katika mikoa ya Kusini na Nyanda za Juu Kusini Magharibi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo jana, mikoa itakayoathirika na mvua hizo ni pamoja na Lindi, Mtwara, Ruvuma, Mbeya, Njombe, Iringa na Rukwa.
Pia, imesema mvua hizo zinaweza kujitokeza katika maeneo machache katika mikoa ya Pwani, Morogoro na Dar es Salaam.
Taarifa hiyo iliwataka wananchi wa maeneo husika kuchukua tahadhari kwa sababu mvua hizo ni kubwa kwa zaidi ya mililita 50 kwa saa 24 katika siku hizo tatu.
TMA ilieleza kwamba uhakika wa kunyesha kwa mvua hizo ni asilimia 70 na wataendelea kutoa taarifa mara kwa mara.
Sababu ya kutokea kwa mvua hizo inaelezwa ni kutokana na kuimarika kwa ukanda wa mvua katika maeneo husika, hali inayoweza kusababisha maafa kwa watu hususan wanaoishi katika maeneo ya mabondeni.
Mwishoni mwa mwaka jana, TMA ilitahadharisha juu ya kutokea kwa mvua za El Nino nchini ambazo zingeweza kuleta madhara kwa wananchi.
ZeroDegree.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) yatahadharisha mvua kubwa kuanza ndani ya siku 3 kuanzia jana.
Reviewed by Zero Degree
on
1/19/2016 12:34:00 PM
Rating: